Mbappe hajapindisha maneno ameamua tu kuwa mkweli.
Joyce Shedrack
June 22, 2026
Share :
Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian ametoa maoni yake kuhusu muda wa mapumziko wa kunywa maji kwenye kila mechi ya Kombe la Dunia.

"Maoni yangu kuhusu mapumziko ya kunywa maji? Msituulize sisi wachezaji maoni yetu, kwa sababu mara nyingi tunatoa maoni kulingana na hali ya wakati huo.
“Ikiwa kesho tutakuwa tunatawala mchezo kufikia dakika ya 25 na kukawa na mapumziko ya kunywa maji, tutakasirika kwa sababu yatavunja mtiririko wetu wa mchezo”.
"Lakini ikiwa hali ya hewa ni ya joto sana, au sisi ndio tunatawaliwa na wapinzani, basi nitafurahia mapumziko hayo."Amesema Mbappe.





