Mbappe kujiunga Madrid bure
Sisti Herman
February 5, 2024
Share :
Huenda huu ukawa mwisho wa sakata la muda mrefu, lililochukua zaidi ya miaka 5 kwa mshambuliaji wa PSG na timu ya Taifa Ufaransa Kylian Mbappe kuhitaji kujiunga na klabu ya ndoto zake Real Madrid baada ya tetesi kutoka vyanzo mbalimbali barani Ulaya kusema atajiunga rasmi na mabingwa hao mara nyingi wa vilabu barani Ulaya na duniani kwa ujumla.
Tetesi hizo zimebainisha kuwa mara baada ya mkataba wake kuisha mwishoni mwa msimu huu Mbappe atajiunga Madrid akiwa mchezaji huru.