Mbappe kuvuna mabilioni PSG
Sisti Herman
January 18, 2024
Share :
Klabu ya PSG ina mpango wa kuketi mezani na nyota wa klabu hiyo Kylan Mbappe ili waone kama kuna uwezekano wa kumuongezea mkataba mpya nyota huyo.
Mkataba wa awali wa Kylan Mbappe na klabu ya PSG unatarajiwa kutamatika mapema mwishoni mwa msimu huu na kuanzia mwezi wa kwanza alikuwa anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine.
PSG ina mpango wa kumlipa kiasi cha £ 86 Million [Billion 275] kwa mwaka iwapo nyota huyo atakubali kuongeza mkataba mpya na atapokea £ 1.8 Million [Billion 5.7] kwa wiki kumfanya awe nyota anayelipwa zaidi ulimwenguni.
Hadi hivi sasa hakuna makubaliano yaliyofanywa kati ya Mbappe na Real Madrid kama ilivyotajwa hapo awali japo kwa mujibu wa mkataba wake ulipofikia anaweza kuongea na klabu yoyote.