Mbappe mmiliki mdogo zaidi wa klabu Duniani ainunua Bilioni 58.6.
Joyce Shedrack
July 30, 2024
Share :
Mchezaji nyota wa Real Madrid Kylian Mbape amefanikiwa kuinunua klabu ya Caen inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Ufaransa kwa thamani ya Euro milioni 20 sawa na TZS bilioni 58.6.
Mbape ameweka historia ya kuwa mmiliki wa klabu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kutokea katika historia ya mpira wa miguu barani Ulaya akiwa na umri wa miaka 25.
Mchezaji huyo amekamilisha dili hilo siku chache tu baada ya kujiunga na Real Madrid aliposajiliwa kama mchezaji huru na kufanikiwa kuingiza kitita kikubwa cha fedha ambazo ni zaidi ya bilioni 439.2 za usajili wake.