pmbet

Mbaroni kwa kumpiga mhudumu aliyemdai hela ya pombe alizokunywa

Eric Buyanza

February 28, 2024
Share :

Huko Wilayani Tarime Mkoa wa Mara, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Majengo Mapya aliyefahamika kwa jina la Silas Nyamhanga, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum Tarime-Rorya kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi mhudumu wa baa, Jenipher Shaban baada ya kumdai Shilingi 24,000 kama bili ya pombe alizokunywa.
 

Tukio hilo limethibitishwa Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Marck Njera ambaye amesema mtuhumiwa anakabiliwa na tuhuma za kumjeruhi mhudumu huyo kwa kumshambulia kwa rungu, ngumi na mateke sehemu mbalimbali za mwili na kumng'oa meno mawili.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet