Mbele kugumu lakini tutafika mbali - Msuva
Sisti Herman
January 21, 2024
Share :
Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Simon Msuva ameweka wazi kuwa michezo miwili iliyobaki dhidi ya Zambia na DR Congo sio michezo rahisi kwa upande wao.
Msuva ameweka wazi kuwa licha ya kuwa migumu lakini bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwa kuanza na mchezo wa kesho Jumapili, January 21 dhidi ya Zambia.
“Mimi naamini timu yetu ni nzuri, naamini tutafika mbali kwasababu bado tuna nafasi, tumebakiza michezo miwili, michezo ambayo ipo mbele yetu sio rahisi”, ameongea Simon Msuva, mchezaji wa Stars.
Tanzania ilianza kwa kupoteza kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya timu ya Taifa ya Morocco na sasa wanaangalia namna ya kupata alama kwenye michezo inayofuata.