pmbet

Mbinu za De La Fuente zilivyozima utawala wa Argentina ya Scaloni na Messi.

Sisti Herman

July 21, 2026
Share :

 

Utangulizi


Timu ya taifa ya Hispania imetwaa Ubingwa wa kombe la dunia baada ya kuweza kuifunga timu ya taifa ya Hispania goli 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Metlife jijini New York nchini Marekani.

 

 

Fainali ya Kombe la Dunia kati ya Hispania na Argentina haikuwa mechi ya ushindani wa kushambuliana pande zote mbili, bali ilikuwa vita ya kimbinu kati ya timu iliyotawala mchezo kupitia umiliki wa mpira na nafasi (territorial dominance) ambayo ni Hispania chini ya kocha Luis De La Fuente, dhidi ya timu iliyojipanga kulinda eneo lake kwa nidhamu kubwa (organized low block) ambayo ni Argentina ambayo ipo chini ya kocha Lionel Scaloni.

 

Kama walivyofanya kwenye michuano hadi mwisho wakimaliza na magoli 14 ya kufunga na goli moja la kufungwa kwenye mechi 8, kwa dakika zaidi ya 100 dhidi ya Argentina, Hispania ilionekana kuwa timu iliyokuwa na udhibiti kamili wa mchezo kwa kumiliki mpira kwa zaidi ya 60% hasa kwenye theluthi mbili za mwanzoza uwanja kutoka langoni mwao kwa pasi fupi na ikitengeneza nafasi nyingi za kufunga kwenye theluthi ya mwisho ambapo kati ya mashuti 20 waliyopiga, mashuti 12 yalilenga lango la Emiliano Martinez na moja lilizaa goli la ushindi.
 

 

Lakini kama ilivyokuwa falsafa yao ya kuzuia walitumia umiliki huo wa mpira kuisukuma Argentina karibu kabisa na eneo lao la kujilinda na kila Argentina walipopora umiliki wa mpira au walipokuwa na mpira walizuia kwa shinikizo kubwa sana ili kuurudisha umiliki wa mpira kuwa wao (Counter Pressing/Pressing).

 

 

Argentina ilitegemea zaidi uimara wa safu ya ulinzi na ubora wa kipa Emiliano Martínez ambaye kwenye mchezo huo aliokoa jumla ya hatari 11 (saves) na Mwishowe, presha ya Hispania ilizidi uwezo wa Argentina kuhimili, na bao la Ferran Torres katika dakika ya 106 likawa tofauti iliyowapa Wahispania ubingwa wao wa pili wa Kombe la Dunia.

Argentina ilitegemea mashambulizi ya kujibu (Offensive Transitions) kama njia ya kuishambulia Hispania wakimtegemea Messi kama mchezaji anayebaki mbele kwaajili ya kupokea mashambulizi hayo ya kujibu kama alivyofanya kwenye michuano hii kutoshiriki matukio mengi ya kiuzuiaji ili kuwa sehemu ya timu yake kutoka wakati wa mashambulizi ya kujibu (Rest Attack) lakini hawakufanikiwa kutokana na ubora wa Hispania kukabilia na mashambulizi ya kujibu (Difensive Transitions) kiasi cha kutowaruhusu Argentina kutenegeneza nafasi nyingi na wakamaliza mchezo bila shuti lolote lililolenga lango.

 

 

Vita ya Mbinu kati ya De La Fuente na Scaloni. 

 

Hispania walitumia mfumo wa 4-2-3-1 huku Argentina wakitumia mfumo wa 4-4-2, kwasababu nyakati nyingi Hispania walikuwa na mpira hasa kwenye nusu ya Argentina, walinyumbulisha mfumo wao kuwa kwenye muundo huu;
 

 

 - Rodri alicheza mbele ya mabeki wawili wa kati, Laporte na Cubarsi nyakati nyingi ili kuweza kupkea na kuendeleza mashambulizi kwenye njia zote za kati na pembeni na kutawala umiliki wa mchezo kwa pasi zake fupi (Build up progressions & tempo controller)

 

 

 - Yamal na Cucurella walicheza pembeni kwenye mapana ya uwanja (Flanks) ili kutanua kuta za uzuiaji za Argentina kwenye pembeni na kutengeneza mianya kwenye chaneli za ndani kwaajili ya Pedro Porro na Baena (Half Spaces)

 


 - Fabien Ruiz na Dani Olmo waliunganisha wachezaji wa pembeni (Half Spaces & Flanks) na kutengeneza pembetatu pembeni mwa uwanja zinazorahisisha flow ya pasi na kutopoteza umiliki wa mpira na hata wakipoteza iwe rahisi kuanza kuurudisha kwa haraka kwao kwasababu huwa wengi eneo moja.

 - Oyarzabal alikuwa kama mtu wa ziada ule upande shambulizi linapotokea kuongeza idadi na kusaidia timu kuweza kupenya kuta za uzuiaji za Argentina kwa urahisi kwa kutumia idadi kubwa yeye akiongezeka (Freeman/Third Man Runner)

 

 

Mbinu kubwa ya Luis de la Fuente ilikuwa kutumia ubora wa upande wa kulia ambapo Pedro Porro alipanda mara kwa mara kutoka nafasi ya beki wa kulia na kushirikiana kwa karibu na Lamine Yamal.

Ushirikiano wao uliunda hali nyingi za 2 dhidi ya 1 dhidi ya Nicolás Tagliafico na Kutokana na hali hiyo:

 

 - Hispania waliweza kufungua nafasi za kupiga krosi.

 - Waliivuta safu ya kiungo ya Argentina kuelekea pembeni.

 - Walipanua defensive block ya Argentina na kuacha nafasi maeneo mengine.

  •  

Kwa muda mrefu Argentina walifanikiwa kuhimili mashambulizi hayo, lakini presha iliendelea kuongezeka hasa baada ya De La Fuente kufanya mabadiliko ya wachezaji walioongeza nishati na ufanisi kama Nico Williams na Ferran Torres na hatimaye bao la ushindi lilitokana na mpangilio huo huo.

 

Yamal alitanua na mpira kwenye mapana ya uwanja na kutanua ukuta wa Argentina, akarudisha mpira kwa Pedro Porro aliyekuwa kwenye Half Space.


Kisha Pedro alitoa krosi kutoka kulia kuelekea kwenye box na Nico Williams akaurudisha mpira mbele ya lango kwa kichwa, kabla Ferran Torres hajamalizia kwa shuti la kwanza.

 



Ni bao lililotokana moja kwa moja na style ya uchezaji na mfumo ambao Spain walikuwa wameutumia karibu mchezo mzima.
 

Argentina hawakupiga shuti hata moja golini

 

Lionel Scaloni aliingia na mpango wa kulijilinda zaidi ambapo mbinu yake bora kushambulia ilikuwa ni kushambulia kwa mashambulizi ya kujibu wakitegemea zaidi Messi kama muongoza wa nyakati hizo ambapo huwa huachwa nyakati za kuzuia ili wakipora mpira wampe yeye aweza ku-drive mashambulizi ya kujibu (Rest Attack) lakini walikutana na timu bora kuzuia mashambulizi ya kujibu ambayo ni Hispania waliweza kuizuia Argentina kupiga shuti kulenga lango lao kwenye mchezo mzima huku wakiambulia mashuti mawili tu yasiyolenga lango kwenye dakika za nyongeza.
 


Hispania wakipoteza mpira walikuwa bora kuzuia mashambulizi ya kujibu na kuurudisha mpira kwenye utawala wao ambapo kwenye mchezo huo walikuwa na  wastani wa kuruhusu Argentina kupiga wastani wa pasi 8.2 na kuanza kuzuia kwa presha kubwa na kuwapora mpira kisha kuurudisha kwenye umiliki wao (PPDA 8.2, Passes Per Difensive Actions).
 

 

Hali iliyowafanya kushindwa kufika kwenye theluthi ya mwisho ya Hispania, ambapo kwenye mchezo mzima waliweza kufika mara 39 tu kabla ya dakika za nyongeza.

Hispania kwenye michuano hii ni moja kati timu zenye umbo zuri linalomeza mashambulizi ya kujibu ya timu zinazofanya mashambulizi ya kujibu ambapo mar azote Rodri husimama mbele ya mabeki wake kwaajili ya kulinda wasifikike kirahisi pindi timu ikipoteza umiliki wa mpira kwa wachezaji wa mbele (Rest Defence) huku wakianza kuzuia kwa presha kubwa pale wanapopoteza mpira ili kuurudisha kwenye umiliki wao (Counter Pressing)
 

 

Kadi Nyekundu ya Enzo Fernández Ilibadilisha Mchezo

 

Dakika za mwisho za muda wa kawaida zilikuwa sehemu muhimu ya mchezo, Enzo Fernández alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupata kadi ya pili ya njano, Hapo ndipo mfumo wa kujilinda wa Argentina ulianza kuporomoka.

 

Kabla ya hapo tayari Scaloni alikuwa amemtoa Julián Álvarez na kumwingiza Marcos Senesi ili kuongeza beki wa tatu wa kati, Lengo lilikuwa kufika kwenye mikwaju ya penalti.

 

Lakini baada ya kubaki na wachezaji 10:

 

 - Defensive block ilipungua nguvu.

 - Umbali kati ya wachezaji ukaanza kuongezeka.

 - Walishindwa kutoka kwenye presha ya Spain.

 - Walishindwa pia kuondoa mipira kwa utulivu.

 

Spain waliinua presha mara moja, Ndani ya dakika moja ya kipindi cha pili cha muda wa ziada kuanza, bao likapatikana.

Wachezaji nyota wa Hispania



1. Rodri - Mchezaji bora wa michuano

 - Ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya kombe la dunia ambapo kutokana na uwezo wake wa kiufundi alikuwa nyota wa Hispania aliyechangia kwa kiasi kikubwa mbinu za kocha De La Fuente kutimizwa dimbani hasa uwezo wa kutawala umiliki wa mchezo kwa kupiga pasi sahihi nyingi na kuweza kuwalinda mabeki wake kwenye nyakati za mashambulizi ya kujibu.

 

 - Kitakwimu wa mchezaji aliyepiga pasi nyingi kwa timu yao akipiga pasi 799 kati ya pasi 5470 za timu nzima na pia amekuwa mchezaji aliyekimbia umbali mrefu ndani ya dimba kwa timu yao akikimbia kilometa 96.23.

2. Unai Simon - Kipa bora wa michuano

- Amekuwa mhimili muhimu kwa timu hiyo ambapo kwenye michuano hii ndiyo kipa aliyecheza dakika nyingi na kuruhusu kufungwa idadi ndogo zaidi ya magoli.

 

 - Kitakwimu Unai ameruhusu goli 1 tu kwenye mechi 8 huku akipata hati safi (Clean Sheets) 7 na kufanya Saves 14 pia ameweza kufanya jumla ya matendo 120 ya kiuzuiaji ndani ya box na mengine 93 nje ya box.

3. Paul Cubarsi wa michuano

- Beki huyu wa kati amekuwa nguzo muhimu kwa timu hiyo ambapo ameweza kuisaidia kumaliza mechi 8 za kombe la dunia ikiwa na Clean Sheet 7 huku akitimiza majukumu ya kiuzuiaji na kiushambuliaji kwa kiwango cha juu sana.

Hitimisho

 

Hispania chini ya kocha Luis De La Fuente wameonyesha kiwango cha timu iliyojiandaa vizuri kushindania Ubingwa kwasababu imeonyesha ubora wa juu zaidi ambapo kwenye michezo yote 8 ya kombe la dunia wamefunga magoli 14 na kufungwa goli 1 pekee.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet