pmbet

Mbinu za Ibenge Azam FC zilivyoiadhibu JKT ya Hamad Ally

Sisti Herman

April 17, 2026
Share :

 

Utangulizi 

 

Azam FC imeibuka na ushindi goli 3-0 nyumbani dhidi ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa raundi ya 19 a Ligi Juu Tanzania msimu wa 2025/26 uliochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

 

Takwimu za mchezo

 

Kwenye mchezo huo, Azam FC kuanzia mwanzo wa mchezo walionyesha utawala wa mchezo ambapo hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza walitawala mchezo kwa umiliki wa mpira wa 71% huku wakitengeneza nafasi 14 za kufunga na kuweza kupiga mashuti matano yaliyolenga lango bila kuambulia goli.

 

Hizi ni takwimu za kipindi cha kwanza zilizokusanywa na Soka Metrics.

 

 

Kipindi cha pili inaonekana Kocha Florent Ibenge na wasaidizi wake walifanya tathmini sahihi ya namna ya kuboresha matendo kwenye theluthi ya mwisho (final third) hasa umaliziaji wa nafasi nyingi zilizotengenezwa na vijana wake na walivyorejea wakaweza kuzitumia kwa usahihi wakidumisha utawala wa mchezo kwa 61%, wakitengeneza nafasi zingine 7 za kufunga huku kati ya mashuti manne yaliyolenga lango kipindi cha pili, matatu yakiwa magoli.

 

Hizi ni takwimu za mchezo mzima zilizokusanywa na Sola Metrics.

 

 

Mbinu za Ibenge zilizozamisha jahazi la vijana wa Hamad Ally

 

Vikosi

 

Kwenye 'line ups' za timu zote 2 makocha waliingia na vikosi hivi hapa kulia;
 

Azam FC ilitumia nyakati 3 uwanjani kuimaliza JKT Tanzania

 

1. Ikiwa inashambulia (In Possession moments)

 

Azam wakiwa na mpira walicheza na mfumo wa 4-2-3-1 ambapo;

 

- Ujenzi wa shanbulizi ulihusisha pasi fupi kutoka kwa Manula, Fuentes na Yoro ili kujaribu kuwavuta JKT kwenda kuzuia kuanzia mbele na kutengeneza mianya katikati au nyuma ya ukuta wao

 

- Uendelezaji wa shambulizi ulitegemea zaidi njia 2, katikati kwa Akamiko na Himid Mao au pembeni kwa Lusajo na Msindo, hii ilitegemeana na namna JKT wanavyozuia

 

- Wakiwa kwenye nusu ya JKT, Azam walinyumbulisha muundo wao kwa kutawanya wachezaji kwenye mikondo mitano ya uwanja ili kuweza kuwatanua 

 

JKT kwenye mapana ya uwanja na kupenya ukuta wao na kufika kwenye theluthi ya mwisho ya uwanja

 

JKT nao walikuwa wakizuia na mfumo wa 4-4-2 ambapo mistari yao ya uzuiaji ilikuwa na;

 

- Mstari wa mbele wawili, Kapalata na Mudi Beka
- Mstari wa kati watu wanne, kati Nassor na Msengi na pembeni Karabaka na Kasunda
- Mstari wa mwisho watu wanne, kati Paschal na Makame na pembeni Anuar na Brayson

 

Kwasababu JKT walizuia njia za pasi za kati (Passing through the block) hasa kutoka kwa Himid na Akamiko kwenda kwa wachezaji wa mbele ikabidi kwenye moment ya goli la kwanza Azam kutumia ushirikiano wa wachezaji pembezoni mwa uwanja (Passing Around the Block) ili kuweza kupenya kuta za uzuiaji za JKT Tanzania zilizokuwa zimefinya uwanja katikati ya uwanja (Mid Block)
 

 

Kwenye picha utaona namna Azam walitimiza mpango huu kwa kuwatanua JKT kwenye mapana ya uwanja kisha wachezaji wao kushambulia mikondo mitatu ya upande wa kushoto;

 

 

- Iddi Nado anatanua pembeni (Flank/ Wide Channel) na kupokea mpira kutoka nyuma kisha ukuta wa JKT unatanuka na kutengeza mianya

- Feisal anashambulia kati ya beki wa pembeni aliyemfuata Nado na beki wa kati aliyebaki (Half Space/ Inside Channel) kisha kupokea mpira kutoka kwa Nado

- Kitambala bola aliyekuwa kwenye Channel ya katikati anashambulia nafasi kati ya beki wa kati aliyemfuata Feisal na beki wa kati aliyebaki kisha kumalizia kwa usahihi krosi iliyopigwa na Feisal

 

 

 

Mapungufu ya JKT ni namna block yao ilivyotanuka kirahisi na kutengeneza mianya huku wakizuia kwa idadi ndogo channels za pembeni

 

2. Azam FC ikizuia na kujibu shambulizi (Defensive to Offensive Transition)

 

Azam FC ikizuia walizuia na muundo wa 4-4-2 ambapo;

 

- Mstari wa mbele wawili, Kitambala na Feisal huzuia mabeki wa kati wa JKT kutowasiliana na viungo wao
- Mstari wa kati watu wanne, kati Akamiko na Himid huzuia viungo wa JKT kutokuwa huru katikati ya mistari na pembeni Nado na Aba kuzuia mabeki wa pembeni wa JKT kutokuwa huru kushambulia mapana ya uwanja
- Mstari wa mwisho watu wanne, kati Fuentes na Yoro na pembeni Lusajo na Msindo

 

Walizuia kwa shinikizo kubwa hasa kuanzia theluthi ya katikati kutoruhusu JKT kupita na kuwafikia Kirahisi kisha kuwapora mipira na kujibu mashambulizi kwa haraka kabla JKT hawajarejea kwenye muundo wao mzuri wa kuzuia

 

 

Kwenye goli la tatu la Azam FC lililofungwa na Iddi Nado, JKT walikuwa na mpira kwenye theluthi ya katikati ya uwanja wakipita upande wa kulia wa Azam, Akamiko na Lusajo kwa kushirikiana wakapora mpira na haraka haraka kujibu shambulizi kabla ya JKT kuurudisha kwenye utawala wao huku wakimpa Feisal aliyekuwa nyuma ya viungo wa JKT na kuweka pasi nyuma ya mabeki wa JKT akimlenga Kitambala ambaye alimtengenezea goli Nado

 

 

Mapungufu ya JKT yalikuwa staili yao ya kucheza pasi fupi kwa ufanisi mdogo kwenye maeneo finyu yenye presha ya Azam huku wakishindwa kuanza kuzuia kwa presha kubwa pindi mpira unapopotea na pia wachezaji wao kushindwa kuhimili nafasi kubwa nyuma ya mabeki wao

 

 

3. Mipira ya kutenga (Set Plays - Free kick)

 

Azam pia wameweza kutafsiri kwa vitendo tafiti za mpira wa miguu zinazoonyesha kuwa 30% ya magoli kwenye mpira wa miguu hufungwa kwa mipira ya kutenga ambapo leo wameweza kupata goli kwa free kick ambapo Feisal alimuanzishia Freekick Nado aliyekuwa anajongea kutoka mbali bila kuwa marked na mchezaji wa JKT na kupiga shuti la mbali nje ya box

 

 

Mapungufu ya JKT yakiwa kumpa uhuru Iddi Nado na pia kipa wao kushindwa kuhimili shuti la umbali mrefu

Shukrani:
Takwimu; Soka Metrics

Picha; Azam Media

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet