pmbet

Mbinu za kocha Ouahbi zilizowapa Morocco U-20 Kombe la dunia

Sisti Herman

October 20, 2025
Share :

 

Utangulizi

 

Timu ya Taifa ya Morocco u-20 imetwaa taji la kombe la dunia ikiifunga 2-0 timu ya taifa ya Argentina kwenye mchezo wa fainali uliochezwa alfajiri ya kuamkia leo, Santiago, Chile.


Nilibahatika kufuatilia baadhi ya mechi za vijana hao wa kocha Mohamed Ouahbi kama zifuatazo;

 

vs Brazil, walishinda 2-1

vs Spain, walishinda 2-0

vs France, sare ya 1-1, wakashinda kwa matuta 5-4

Na kuanzia hapo niliweza kuandaa Ripoti ya mbinu za uchezaji za timu hiyo zilizowapa taji.

 

Mbinu zipi zimewapa Ubingwa wa dunia?

 

 

Kwenye mechi hizo niliona ni timu inayocheza staili ya uchezaji ya kuvutia kwa mbinu bora za ujenzi wa shambulizi kuanzia nyuma kwenye lango lao kwa pasi za haraka na ufanisi mzuri kuelekea kwenye nusu ya wapinzani wao huku wakizuia kwa shinikizo dogo nyakati nyingi kwenye theluthi ya kati ya uwanja (mid block)

KUSHAMBULIA

 

Muundo wa timu wakati wa Build up ulikuwaje?

 

Morocco alitumia mfumo wa 4-2-3-1 ambao wakati wa Build up ulinyumbulika kuwa kwenye miundo tofauti kama;

 

1. Theluthi ya kwanza ya uwanja wakimhusha kipa 3-4-4

 

Mstari wa kwanza wa ujenzi wa mashambulizi huwa na watu watatu, kipa Benchaouch na mabeki wawili wa kati, Baouf na Bakhty

 

  • - Hawa huhusika kwenye ujenzi wa mashambulizi kuanzia kwenye theluthi ya kwanza ya uwanja, kwenye muundo wa watu watatu au -3- kwenye 3-4-4 (Build up phase)

     

  •  

Mstari unaofuata huwa na watu wanne, viungo wawili wa kati Essadak &  Khalifi pamoja na mabeki wa pembeni, Maamar kushoto & Zahouani kulia

 

- Hawa huhusika kwenye uendelezaji wa mashambulizi, kwa njia mbili, kati na pembeni kulingana na presha ya wapinzani ili kuuvusha na kufika kwenye theluthi ya pili ya uwanja (Progression) 

 

Mstari wa mwisho huwa na viungo washambuliaji wa pembeni wawili, Maamma kulia & Yassine kushoto na washambuliaji wa kati Haddad na Zabiri

 

- Hawa huhusika na kupenya, kutengeneza nafasi na kufunga ambapo viungo washambuliaji wawili wa pembeni hutanua pembeni zaidi, washambuliaji wa kati hugawana, mmoja hushuka katikati ya mistari na mwingine hushambulia nyuma ya mistari ya wazuiaji au wakati mwingine husogea katikati ya msitari wote wawili ili kuwavuta wapinzani na kuacha nafasi kubwa nyuma yao itakayoshambuliwa na viungo wa pembeni (Penetration, Creation and Finishing)

 

Mistari miwili ya mwanzo, yenye wachezaji 6 (7 na kipa) huwa karibu zaidi na goli lao, kwaajili ya kujenga na kuendeleza shambulizi (Build up and progression) huku Mstari wa mwisho wenye watu wanne, mawinga na washambuliaji ukibaki mbele zaidi ili kuwalazimisha mabeki wa timu pinzani kuendelea kubaki nyuma (pinning back) na Kutengeneza nafasi kubwa Katikati ya mistari

 

 

2. Theluthi ya kati na ya mwisho bila kumhusiaha kipa 2-4-4

 

Wakiwa kwenye theluthi mbili za mbele, yaani ya Kati na ya mwisho hawamhusishi kipa wao kwenye build up zao

 

Lengo la Morocco kufanya Build up kuanzia nyuma ni lipi?

 

 

Lengo kuu la Morocco kujenga mashambulizi kuanzia nyuma ni kuwavuta wapinzani kwa kuwashawishi kushinikiza kuanzia kwao ili kutengeneza kina kikubwa cha uzuiaji kwenye kutanua kuta zao za uzuiaji ambacho kitatengeneza nafasi katikati ya mistari au nyuma ya ukuta wao



 Kisha kutumia faida tatu kuwafikia, ambazo ni;

 

(i) Idadi - Faida ya idadi kwenye kila mstari dhidi ya wapinzani, wao wakifaidika zaidi na uwepo wa kipa kwenye mstari wa Kwanza (Numerical Superiority)

 

mfano: dhidi ya Spain waliokuwa wakizuia na muundo wa 4-4-2 (diamond), wao huwa na faida kwenye mstari wao wa kwanza wa uzuiaji wenye watu watatu dhidi ya ule wa wapinzani wenye watu wawili (3v2), au kwenye mstari wa pili kuwa na watu wanne dhidi ya watatu wa Spain hali iliyotengeneza situation ya wawili dhidi ya mmoja kwa kiungo wao kwenye mstari wa pili wa uzuiaji (2v1)

 

 

(ii) Ubora - Faida ya uwezo Kutokana na uwezo wa kiufundi wa wachezaji wa kupiga pasi na kukukokota kwenye nafasi (Qualitative Superiority)

Mfano: hii hapa ni Passing Map ya kipa wao Benchaouch ambaye ndiye Playmaker wa timu kwenye Moment za build up kutokana na uwezo wake kwenye Distributions

 

 

(iii) Nafasi - Faida ya nafasi za kuwafika kwenye lango la wapinzani kirahisi kwa kutumia njia za zinazotokana na nafasi za wazi katikati ya mistari au nyuma ya mstari wa mabeki baada ya kuwavuta kwao (Positional Superiority)

 

 

Njia kuu za Build up za Morocco ni zipi?

 

1. Njia ya kati (Passing Through The Press)

 

Morocco hupenda kuwatumia viungo wawili wa kati Essadak &  Khalifi (double pivot) kama njia ya kwanza ya kupokea na kuendeleza shambulizi linalojengwa na kipa na mabeki kuanzia nyuma kwa kipa na mabeki wawili, hasa pindi wapinzani wanapozua na stili ya mtu dhidi ya mtu (Man Marking) ambayo huruhusu mianya katikati ya mistari yao ya uzuiaji (build up progressions)

 

 

2. Njia ya pembeni (Passing Around The Press)

 

Pindi njia ya kati inapokuwa imezuiwa vizuri kwa wapinzani ku-press na nidhamu nzuri ya kufinya uwanja na kuwakaba mtu na mtu na nafasi (Zonal Marking)  kwa Viungo hao wawili wa kati, Morocco hupenda kuendeleza mashambulizi kwa kutumia mabeki wa pembeni, Maamar kushoto & Zahouani kulia
 

 

3. Njia ya juu - (Passing Over The Press)

 

Wapinzani wanapokuwa wamezuia njia mbili muhimu za Morocco kuendeleza mashambulizi, kwa kuzuia kwa idadi kubwa na kubana uwanja vyema, Morocco hutumia njia za juu kwa pasi ndefu kutoka nyuma, ambapo washambuliaji wao wawili, Haddad na Zabiri husogea hadi Katikati ya mistari ya uzuiaji ya wapinzani ili kuwavuta mabeki wa kati wa wapinzani na kutengeneza nafasi nyuma yao ambayo hushambuliwa na viungo washambuliaji wa pembeni, Maamma kulia & Yassine kushoto

 


 

Mambo muhimu kwenye Build up za Morocco ni yapi?

 

1. Pressure Attraction - kama ilivyo kwa Lengo lake la kujenga mashambulizi kuanzia nyuma, Lengo la kwanza la Morocco ni kuwashawishi wapinzani kuwafuata ili kutengeneza nafasi kuwafikia kirahisi

 

2. Superiority - Baada ya kuwashawishi wapinzani kuwafuata, ni ngumu kutoka kwenye Pressure na kuvunja mistari yao ya uzuiaji bila kuwazidi kwa idadi, ubora, hivyo Morocco kwenye kila eneo mpira ulipo huhakikisha wachezaji wake wapo kwa idadi kubwa na kutumia ubora wao wa kiufundi ipasavyo kama kupiga pasi sahihi na kukokota kwenye nafasi za wazi

 

3. Third Man runner - Baada ya kuwa wengi kwenye eneo dogo lenye mpira, Morocco hutumia mtu wa tatu kuutoa mpira kwenye pressure, kwani huamini mchezaji wake mwenye mpira na wale waliokaribu kupokea mpira huwa kwenye shinikizo kubwa la wapinzani hivyo huhimiza wakati wachezaji hao hupasiana (mwenye mpira na anayetegemea kupokea) kuwepo na mchezaji wa tatu ambaye anakuwa kwenye nafasi  ya wazi nyuma wapinzani ili kuwa tayari kupokea pasi kutoka kwa anayepewa na kuutoa mpira kwenye pressure na kuvunja mistari wa wapinzani

 

4. Vertical Movement - Pindi wachezaji wanapopasiana, kama nilivyoeleza juu, Mwenye mpira, anayetarajia kuupokea na Yule wa tatu anayetegemea kupokea (third man runner), wachezaji hao wote mikimbio yao na mpira ni lazima iwe inaelekea kwenye lango la wapinzani ili kuweza Kutengeneza nafasi za kufunga

Transitions

Kuna zile Moments wameshindwa kuwa wafanisi walijitajihidi sana kuanza kuzuia pale wanapopotezea mpira (Counter Pressing) ili kutoruhusu kufanyiwa shambulizi la Kujibu (Counter Attack) au kuweza kuzuia na kupora mpira na kujibu tena shambulizi

 


UZUIAJI

 

Morocco wakati wa kuzuia, hupenda zaidi kuzuia kwenye theluthiy kati ya uwanja (Mid Third) na mfumo wa 4-4-2, ambapo mistari ya uzuiaji huwa;

- 1st line: Haddad na Zabiri
- 2nd line: Maamma kulia & Yassine kushoto pembeni na Essadak &  Khalifi, kati
- 3rd line: Maamar kushoto & Zahouani kulia pembeni na Baouf na Bakhty Kati



 Muundo huu umewapa balance kuzuia njia za kati na pembeni za wapinzani wao, ambapo;

- Haddad na Zabiri huzuia build up za wapinzani kupita Kwa njia za kati kwa kuvunja mawasiliano Kati wanaojenga shambulizi na wanaoendeleza shambulizi (Build up Phase)

- Essadak &  Khalifi huzuia viungo wa kati wanaoweza kupokea na kuendeleza build up Katikati ya mistari (build up progressions)

- Maamma kulia & Yassine huzuia full backs wa wapinzani kuendeleza shambulizi kwa njia za pembeni, pia hu-track mikimbio yao ili wasitengeneze wide Overloads, yaani Full-backs wao Maamar kushoto & Zahouani wasizidiwe idadi na Full-backs na Wingers wa wapinzani

- Wapinzani wakipita juu, Baouf na Bakhty wapo vizuri kushinda kila situation za duels, juu au chini

 

Pia walikuwa na depth fupi sana ya uzuiaji (umbali kutoka mstari wa nyuma wa uzuiaji hadi wa mbele) haukuzidi mita 40

 Sifa za mbinu za Arsenal kwenye muundo wao wa uzuiaji ni Kama;

- Recovery runs Bora - wachezaji wao kurudi kwa haraka kwenye shape pindi wasipokuwa na mpira
- Compactness - kudumisha muundo wakiwa pamoja Bila gapes kubwa
- Winning duels - Wachezaji wa Arsenal wapo Committed sana kushinda kila situation za kugombania mipira
- Pia walikuwa na kipa mzuri golini kwenye kufanya Saves lakini pia as Sweeper

Wachezaji nyota;

1. Mshambuliaji wao wa kati Yassir Zabiri ameibuka kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo akimaliza na magoli matano sawa na Benjamin Cremaschi wa USA,  Naiser Villareal wa Colombia, Lucas Michal wa Ufaransa.

2. Kiungo wao mshambuliaji wa pembeni, Othamne Maamma amekuwa kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo huku akiwa Top Creator wa magoli kwenye michuano akimaliza na asisti 4, akifuatiwa na kiungo mshambuliaji mwenzie wa pembeni wa Morocco, Gessime Yassine aliyemaliza na asisti 3.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet