pmbet

Mbinu za Shime zilizoirejesha Twiga Stars kucheza WAFCON Back to Back

Sisti Herman

November 9, 2025
Share :


Juma moja lililopita timu ya soka ya wanawake ya taifa ya Tanzania ‘Twiga Stars’ iliandika historia ya kufuzu kwa mara tatu kucheza michuano ya kombe la mataifa ya Afrika (WAFCON 2026) wakiwafunga Ethiopia 1-0 ugenini huku wakiwa na jumla ya magoli 3-0 kwenye mechi zote 2 za kuwania kufuzu michuano hiyo.

 

Nimetumia magoli yote matatu ya Twiga Stars dhidi ya Ethiopia kwenye mechi zote 2 kuelezea mbinu zinazotambulisha kocha mkuu wa Twiga Stars Bakari Shime ‘Mchawi mweusi’ kuanzia;

 

 - Miundo/ mifumo ya uchezaji (Systems of Play)

-  Staili za uchezaji (Style of play)

- Misingi ya uchezaji (Principles of Play)

 

Ya timu yake anayoitumia mara kwa mara kwenye nyakati zote uwanjani kuanzia

- Wakiwa na mpira (In Possession)
- Wasipokuwa na mpira (Out of Possession)
- Nyakati za mpito (Transitions offensive/difensive)

1. Uzuiaji mzuri
(Difensive Organization Out of Possession)

Kwenye goli la kwanza la Twiga Stars kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza lililofungwa na Aisha Mnuka, ubora wa Twiga Stars kwenye goli hilo ulikuwa kuanzia namna wanavyozuia mpira unapokuwa kwa wapinzani wao



- Huwa kwenye muundo wa 5-3-2, hii ikiwa mistari ya uzuiaji;

(i) Backline, mabeki watano, watatu kati, Maseke, Julietha na Katunzi, Wawili Pembeni yao kuna Donisia na Enekia
(ii) Midline, viungo watatu, Pangamwene, Diana & Aisha
(iii) Frontline, washambuliaji wawili Jamila & Opa



- Ethiopia waliokuiwa na mpira walikuwa kwenye umbo la 4-3-3, Twiga Stars wakawazidi hapa;

(i) Idadi kwenye mstari wa mwisho, 5v3
(ii) Wakawa mark kila mmoja kwenye mstari wa viungo wao (Man Marking) ikawa 3v3

- Twiga Stars wakaweka presha kwenye mpira kuwanyima muda na nafasi na kisha wakawapora mpira

2. Kujibu shambulizi
(Offensive/Positive Transition)

- Baada ya kupora mpira Twiga Stars wakafanya shambulizi la kujibu



- Zingatia reaction ya wachezaji baada ya kupora mpira, Uharaka wa kushambulia nafasi kabla Ethiopia hawajarudi kwenye muundo wao wa uzuiaji

- Ufanisi wa matendo, Interception ya Pangamwene, pasi ya Diana, mikimbio ya Enekia, Combo ya Opa, Jamila na Aisha




3. Ujenzi wa shambulizi
(Build up from Back)

Kwenye magoli mawili, goli pekee la ugenini lililofungwa na Diana Lucas na goli la pili la nyumbani ubora wa Twiga Stars ulikuwa kwenye jinsi wanacheza wakiwa wanamiki mpira;

 Goli la nyumbani

(Short Pass build up & Counter Pressing)


- Twiga Stars wakiwa wanajenga shambulizi huwa na muundo wa 3-5-2

 



- Mabeki watatu wa kati huhusika na ujenzi wa shambulizi kuanzia nyuma

 


- Wachezaji watano huhusika na shambulizi kuendelezwa, kupenya kuta za wapinzani na hata kutengeneza hadi kwenye theluthi ya mwisho, kwa njia 2;

(i) Kati, kwa viungo wa kati Pangamwenye, Diana na Aisha
(ii) Pembeni, kwa Wing backs, Donisia na Enekia



- Kwenye goli, Ethiopia waliwa mark viungo wa kati (man marking) kisha wakaacha nafasi kwa Enekia na Donisia, ikawa rahisi kwa Stars kupita kwa Enekia



 Counter Pressing

- Faida nyingine ya Stars ni namna wachezaji walivyo react mpira ulivyopotea kisha kuupora na kujibu shambulizi na kufunga goli.

2. Goli la ugenini

Long Pass build up)

 

Moja ya silaha ya ujenzi wa mashambulizi ya Twiga Stars ni ubora wa mabeki wao wa kati kupiga pasi ndefu kwa ufanisi mzuri zikiwalenga washambuliaji wao wa kati.

 

Christer akiwa mmoja kati ya mabeki watatu wa kati, anachukua jukumu la kupiga mpira mrefu akimlenga Oppa ambaye ni mmoja kati ya washambuliaji wawili wa kati, Oppah anaulinda vizuri na kumrudishia Diana ambaye ni mmoja kati ya viungo watatu wa kati.

 

 

Kwasababu Ethiopia walikuwa wamezuia vizuri Twiga Stars kupiga kati, Diana anachagua kupita kwa Donisia ambaye ni mmoja kati ya wachezaji wawili wa pambeni kisha anapiga pasi nzuri nyuma ya ukuta wa Ethiopia kumlenga Oppah na kurahisisha utengenezaji wa nafasi unafanywa na Oppah kwa Cutback Pass kwenye penalty inayomaliziwa vizuri na Diana.


Video magoli ya nyumbani haya hapa chini:

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet