pmbet

Mbinu zilivyowapa Ubingwa Ivory Coast mbele ya Nigeria Afcon 2023

Sisti Herman

February 14, 2024
Share :

Utangulizi

 

Timu ya Taifa ya Ivory Coast imetwaa ubingwa wa kombe la mataifa Afrika (AFCON 2023) mbele ya Nigeria, mafanikio yaliyoje kwa kocha kijana wa miaka 40 Emerse Fae ambaye ameichukua siku 13 zilizopita Katikati ya mashindano, kwenye hatua ya mtoano ikiwa imetoka kupoteza alama 6 kati ya 9 za hatua ya makundi na kushinda michezo ya mtoano mitatu mfululizo kuanzia robo fainali, nusu fainali na Fainali.

 

Hii ni tathmini ya mbinu zilizotumiwa na makocha wa timu zote 2;

 

Vikosi

 

  • Nigeri chini ya kocha Jose Peseiro raia wa Ureno walichagua kuanza na wachezaji hawa;

 

• Kipa; Stanley Nwabali (GK)
• Mabeki wa kati; Semi Ajayi (RCB), William Troost (CCB) na Calvin Bassey (LCB)
• Viungo wa kati; Alex Iwobi na Frank Onyeka (Double Pivot)
• Viungo wa pembeni; Ola Aina (RWB) na Zaidu Sanusi (LWB)
• Washambuliaji; Ademola Lookman (LF), Samuel Chukwueze (RF) na Victor Osimhen (CF)

 

Ivory Coast chini ya kocha Emerse Fae walichagua kuanza na wachezaji hawa;

 

• Kipa; Yahia Fofana (GK)
• Mabeki; Kati, Evan Ndicka (LCB) & Odilon Kassounou (RCB) Pambeni, Ghislain Konan (LFB) & Serge Aurier (RFB)
• Viungo; Jean Seri (CM), Frank Kessie (RCM) na Seko Fofana (LCM)
• Washambuliaji; Simon Andigra (RF), Max Gradel (LF) na Sebastian Haller (CF)

 

 

Walichezaje?

 

Nigeria

 

- Kocha Jose Peseiro  raia wa Ureno alichagua mfumo wa 3-4-3 na mfumo wao uwanjani ulinyumbulika kwenye miundo mingine kulingana na hali mchezo kama;

 

Wakizuia  5-4-1

 

- Nigeria Wakizuia mfumo wao wa 3-4-3 huwa kwenye muundo wa 5-4-1 ambapo;

 

 • Viungo wa pembeni Aina na Sanusi (Wingbacks) husogea kwenye mstari wa mwisho wa ulinzi Sambamba na mabeki watatu wa kati Ajayi, Troost-Ekong na Bassey Kutengeneza mstari wa watu watano mbele ya kipa (Back 5)
 • Washambuliaji wa pembeni Chukwueze na Lookman husogea kwenye mstari wa pili wa uzuiaji Sambamba na viungo wa kati 
 • Osimhen huwa mwenye kwenye mstari wa mbele wa uzuiaji

 

- Kwenye muundo huu Nigeria ilijitahidi nyakati nyingi kuwa nyuma ya mpira bila kuwaachiana nafasi kubwa Kati ya mtu na mtu huku nyakati nyingi ikipendelea kuzuia kwenye theluthi mbili za mwisho za uwanja (Mid & Low Block), wakizuia njia za Ivory Coast kupita;

 

 • Katikati, Osimhen akiwa mbele ya Viungo wawili wa kati, huzuia mawasiliano ya mabeki wa Kati wa Ivory Coast na kiungo wa Kati wa Ivory Coast huku nyuma yake viungo wawili wakizuia viungo washambuliaji wa Ivory Coast kutawala eneo mbele ya mabeki wao
 • Pembeni, Viungo wa pembeni Aina na Sanusi (Wingbacks) walimaliza mapana ya uwanja Kuzuia njia za wachezaji wa Ivory Coast wanaopita pembeni kupiga krosi huku Washambuliaji wa pembeni wa Nigeria Chukwueze na Lookman wakirudi mbele ya Wingbacks wao kuzuia viungo au washambuliaji wa Ivory Coast wasiende kuwazidi idadi maeneo ya pembeni (Wide Overloads)
 • Juu, Pindi Ivory Coast walipochagua kupita njia za juu, mabeki watatu wa kati wa Nigeria Troost-Ekong, Ajayi na Bassey walijitahidi kushinda mipira ya juu inayoelekezwa hasa kwa washambuliaji wa Ivory Coast kisha viungo wao kuokota mipira ya pili na kuanzisha shambulizi

 

- Kwenye aina hii ya uzuiaji Nigeria walijitahidi sana kuzuia kwenye muundo sahihi, kuweka presha kwenye mpira kwa nyakati nyingi huku pia wakitumia nyakati wakipora kushambulia mashambulizi ya kujibu kabla Ivory Coast hawajarejea kwenye muundo wao mzuri wa kuzuia (Positive Transitions) ambapo njia zao za mashambulizi ya kujibu zilikuwa;

 

 • Pasi ndefu za haraka kuelekea kwa Osimhen ambaye alikua kama target man wa timu
 • Lookman na Chukwueze kushambulia nafasi za pembeni kwa haraka
 • Viungo na mabeki kupiga pasi za haraka na sahihi kwenye nafasi

 

Wakishambulia 3-4-3

 

- Nigeria Wakishambulia muundo habadilika kutoka kuwa 5-4-1 na Kutengeneza miundo tofauti mfano;

 

Matumizi ya Back 3

 

- Nigeria Wakishambulia muundo wao huwa na mabeki watatu tu Ajayi, Troost-Ekong na Bassey ambao huwa na jukumu la kujenga mashambulizi kuanzia kwa kipa na kuchezesha timu kuanzia nyuma (ball playing defenders)

 

- Hawa hujenga mashambulizi kupitia njia 3 tofauti;

 

• pembeni kwa Wingbacks Aina na Sanusi pindi Ivory Coast wanapokuwa wamefinya uwanja njianza Katikati
• Katikati kwa Double Pivot Iwobi na Onyeka pindi Ivory Coast wanapokuwa hawajafinya uwanja Katikati
• Juu, Pindi Ivory Coast wanapokuwa wamezuia njia zote za Kati na pembeni, mabeki hawa wa kati hupiga mipira mirefu kwa washambuliaji, aidha Osimhen au Lookman na Chukwueze wanashambulia nafasi nyuma ya mabeki wa Ivory Coast


Matumizi ya Wing-Backs

 

- Nigeria walitumia zaidi viungo wa pembeni Aina na Sanusi kwenye kushiriki Matendo mengi timu yao ikishambulia, mfano;

 

 • Uendelezaji wa mashambulizi (Build up progression)

 

- Wing-Backs wa Nigeria walitumika kusaidia mashambulizi kuendelezwa kwa njia za pembeni pindi Ivory Coast wanapozuia njia za kati kwa usahihi
- Hapa Nigeria walitengeneza muundo wa 3-4-3 (Flat), Wingbacks wakiwa pembeni ya Double Pivot

 

• Upenyaji na utengenezaji wa nafasi

 

- Wingbacks wa Nigeria walitumika kusaidia timu kupenya kwa kushambulia mapana ya uwanja kwenye theluthi ya mwisho ili kusaidia kutanua kuta za uzuiaji za Ivory Coast kutanuka na washambuliaji kupata mianya Katikati ya mistari

- Kama Kuta za Ivory Coast zisipowafuata basi hushiriki Kutengeneza kwa kupiga krosi na pasi za mwisho kwa uhuru

 

Matumizi ya Box Midfield (3-box-3)

 

- Kuna nyakati Nigeria walitengeneza muundo wenye box eneo la kiungo ambayo iliwasiliana kusaidia Uendelezaji, upenyaji na utengenezaji wa nafasi kwa njia za Katikati

 

 • Iwobi na Onyeka walicheza mbele ya mabeki watatu, kusaidia kuendeleza mashambulizi kwa njia za Katikati, positioning zao huwa kati ya mstari wa washambuliaji na viungo washambuliaji wa Ivory Coast 
 • Lookman na Chukwueze Walicheza nyuma ya mstari wa washambuliaji watatu (Wing-backs + Osimhen), Positioning zao huwa nyuma ya mstari wa Viungo wa Kati wa Ivory Coast

 

- Box midfield hii inayocheza kwenye channels, nafasi Kati ya wachezaji wa Kati na pembeni wa Ivory Coast

 

Matumizi ya Target Man

 

- Nigeria imemtumia Victor Osimhen kama mshambuliaji wa kati ambaye jukumu lake kubwa ni kuunganisha timu, mashambulizi mengi kutoka nyuma huelekezwa kwake na yeye ndiyo hushiriki kuwachezesha Wing-backs au washambuliaji wa pembeni

- Kuna nyakati hushuka hadi Katikati ya mistari kuongeza idadi na kushiriki timu kuweza kupenya hadi kwenye theluthi ya mwisho ya uwanja


Ivory Coast

 

Kocha Emerse Fae alichagua kuingia na mfumo wa 4-3-3 ulionyumbulika kwenye miundo mingine kulingana na hali ya mchezo kama;

 

Wakizuia

 

- Ivory Coast ikizuia muundo wao hunyumbulika kwenye miundo mingine kulingana na theluthi mpira ulipo na namna Nigeria wanavyojenga mashambulizi, mfano;

 

• 4-1-4-1 huu muundo Ivory Coast walitumia wakianza kuzuia kuanzia kwenye theluthi ya ujenzi wa mashambulizi ya Yanga (high block), Haller akiwa kwenye mstari wa mbele nyuma yake kukiwa na mstari wa viungo wanne, wawili wa kati Fofana na Kessie dhidi ya Viungo wawili wa Nigeria huku Andigra na Max pembeni Wakizuia Wing Backs wa Nigeria waisendeleze shambulizi

• 4-2-3-1 Muundo huu hunyumbulika kutoka kwenye 4-1-4-1 pindi kiungo mmoja wa kati wa Nigeria anaposogea mbele zaidi, Kessie au Fofana husogea usawa wa Seri kuwa wawili mbele ya mabeki (double pivot)

• 4-5-1 muundo huu waliutumia Pindi wanapozuia kwenye theluthi mbili za ulinzi, Haller mbele kwenye mstari wa kwanza wa uzuiaji, nyuma yake kuna Barrier ya watu watano, Seri, Fofana na Kessie kati Wakizuia njia za Onyeka na Iwobi kuwasiliana na Lookman na Chukwueze, pia pembeni Andigra na Max kuzuia Wingbacks wasilete madhara kwenye mapana ya uwanja

 

- Pia Ivory Coast walikua vyema kuzuia pasi ndefu zinazoelekezwa kwa Osimhen, pia Fullbacks walijitahidi kuzuia Lookman na Chukwueze wasilete madhara

 

- Nyakati ambazo Ivory Coast wakipokonya mpira hujibu mashambulizi haraka (Positve Transition) kwa washambuliaji wa pembeni Andigra na Max hutoka kwenye usawa wa Viungo kwenye 4-5-1 na kushambulia mapana ya uwanja kwa haraka hadi usawa wa Haller na Kutengeneza muundo wa 4-3-3, huku viungo Seri, Kessie na Fofana wakiwa nyuma yao

 

Wakishambulia 4-3-3

 

- Wakishambulia Ivory Coast hutegemea unyumbulifu wa miundo kwenye maeneo tofauti, mfano;

 
 Viungo (Midfield Variations)

 

 Miundo ya Viungo wa Ivory Coast wanaposhambulia huwa kwenye miundo tofauti kama;

 

• Viungo wawili wa Kati (Double Pivot)

 

- Ivory Coast nyakati ambazo Nigeria huzuia wengi na kwa presha kubwa hutumia Viungo wawili wa kati mbele ya mabeki ambapo Fofana au Kessie, mmoja wao husogea usawa wa Seri na kuwa wawili kwaajili ya kuweza kuendeleza shambulizi wakiwa under pressure huku mmoja akiwa nyuma ya mstari wa viungo wa Nigeria kama kiungo mshambuliaji

 

• Viungo wawili washambuliaji (Single Pivot)

 

- Ivory Coast nyakati nyingi Nigeria wakizuia kwenye nusu yao, hutumia kiungo mmoja mbele ya mabeki Seri na wawili washambuliaji Fofana na Kessie

- Seri mara nyingi alibaki mbele ya mabeki kwaajili ya kuzua risk za Counter Attacks za Nigeria pindi timu yao inapopokonywa mpira (Rest Defence)

 

• Kuwa wengi pembeni (Wide Overloads)

 

- Ivory Coast hutumia pia njia za pembeni kupenya kuta za uzuiaji za Nigeria kwakutengeneza pembetatu muhimu pembeni mwa uwanja za Pande zote 2 ambazo huwa na mabeki wa pembeni (Konan & Aurier) na mawinga (Max & Andigra)kwenye mapana ya uwanja wakiunganishwa na viungo washambuliaji wa kati (Kessie & Fofana) waliocheza kwenye nafasi kati ya Viungo wa Kati wa Nigeria na Wingbacks wao (Channels)

 

- Ivory Coast walitumia njia mbalimbali kuweza Kutengeneza nafasi kama;

 • Njia za Katikati kwa Kessie na Fofana Kutengeneza nafasi za kufunga Kwa Haller 
 • Njia za pembeni kwa kutumia wide combination ambazo huzaa krosi za juu au Cutbacks passes kwenye eneo la mwisho
 • Njia za juu hasa Nigeria wakizuia vizuri kwenye theluthi zao mbili za mwisho kwa wachezeshaji wa nyuma wa Ivory Coast, mabeki wa kati au Viungo kupiga pasi ndefu kwa Haller kama Target man

 

MBINU ZILIZOAMUA MECHI

 

Mipira ya kutenga (Set Plays)

 

 Magoli ya mawili ya mchezo yametokana na mipira ya kona, mipira ya kona ni aina ya magoli inayotokana na mipira ya kutenga (Set Pieces) ambayo kwa mujibu wa tafiti mbalimbali huchangia 30% ya magoli yote kwenye soka.

 

Nigeria na Ivory Coast walijitahidi kutimiza kila kitu kwa usahihi kwenye tendo mpira wa kutenga wa kona;

 

  • - Uchaguzi sahihi wa mpigaji, eneo la kuelekeza mpira
    • -Kujitoa na kuhakikisha Kushinda mipira ya juu na inayodondoka (Aerial balls & Second balls)
pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet