pmbet

Mbivu na Mbichi kujulikana tarehe 8/8/2024 Lupaso Kariakoo Derby.

Joyce Shedrack

July 18, 2024
Share :

Ratiba ya michezo ya ufunguzi wa Ligi Kuu michezo ya Ngao ya Jamii imetoka hii leo ambapo mchezo wa Fainali utawakutanisha watani wa Jadi wa Kariakoo miongoni mwa derby kubwa na ya kusisimua barani Afrika itapigwa Lupaso Benjamini Mkapa tarehe 8 mwezi 8 2024.

Mchezo wa Nusu Fainali ya Pili utawakutanisha matajiri wa jiji la Dar es Salaam Azam Fc na wagosi wa kaya Coastal Union mtanange utakaopigwa katika dimba la New Amani Complex Zanzibar siku hiyo hiyo tarehe 8 ya nwezi wa 8.

Msimu uliopita Ngao ya jamii iliwakutanisha Simba na Yanga katika hatua ya fainali zilizochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga mnyama Simba akifanikiwa kutwaa ngao hiyo ya hisani mbele ya mtani wake baada ya kushinda mikwaju 3 dhidi ya 1 wa Yanga.

Mchezo wa mshindi wa tatu na fainali utapigwa 11/08/2024 Benjamin Mkapa kwa majira tofauti.

Timu yako imesajili vizuri ?.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet