Mbosso aiteka mitandao ya kijamii baada ya kutumbuiza kwenye Simba Day.
Joyce Shedrack
September 11, 2025
Share :
Siku ya jana ya Septemba 10,2025 ilikuwa ni tamasha la Simba Day huku wanamsimbazi wakilitaja kama tamasha la kihistoria kutokana na kile walichokifanya katika sherehe hizo.
Staa wa muziki wa bongofleva Mbosso Khan ambaye alikuwa mtumbuizaji mkuu kwenye tamasha hilo ameendelea kuzua gumzo kwenye mitandao ya kijamii kutokana na show ya kibabe aliyoifanya ndani ya dimba hilo la Benjamini Mkapa.
Moja ya jambo ambalo limebaki kuwa gumzo ni namna ambavyo staa huyo alitumia dakika zaidi ya 60 kuimba nyimbo zake na mashabiki wa Simba walioujaza uwanja huo.