pmbet

Mbosso athibitisha kupona ugonjwa wa moyo.

Joyce Shedrack

February 13, 2025
Share :

Staa wa bongofleva Nchini Mbosso Khan amefunguka kuhusu ugonjwa wa moyo uliokuwa unamsumbua muda mrefu huku akiweka wazi kuwa tayari amepona ugonjwa huo baada ya upasuaji aliofanyiwa wa kutibu tatizo lake.

Mbosso amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akitoa shukrani kwa hospitali aliyokuwa anatibiwa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

“Mnamo tarehe 28 mwezi wa 12 mwaka 2024 nilipata nafasi Ya kushiriki kwenye zoezi la upimaji wa Afya Ya Moyo lililofanyika katika Taasisi Ya Moyo Jakaya kikwete (JKCI) Kawe Jijini Dar Es Salaam.. Zoezi hili liliandaliwa na Mheshimiwa Rais @samia_suluhu_hassan kwa ushirikiano wa Taasisi ya JKCI na @basata.tanzania na @tanzania_film_board ikilenga kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu kufuatilia hali ya afya ya moyo na kuzuia magonjwa yanayoweza kuzuilika”

“Kupitia zoezi hili iligundulika ninashida ya Moyo ambayo nilizaliwa nayo kitaalamu niliambiwa ni shida ya Umeme wa Moyo ambayo Taasisi ya JKCI wakishirikiana na Basata waliahidi kunisaidia na kupona kabisa”.

Alhamdulillah Alhamdulillah 🤲🏽

Siku Ya juzi kuja Jana ilikuwa na masaa 12 hadi Kutimia 24 yenye hofu kubwa kwangu ambayo yameleta matoke Ya furaha na amani ya milele kwangu , Familia yangu na kwa Mashabiki wote wa Mziki Wangu

Nilipata nafasi yakutibiwa na Madaktari bingwa kabisa wa Maswala Ya moyo kutokea nchini misri ( Egypt 🇪🇬) sambamba na Madaktari kutoka nyumbani hapa hapa Tanzania ndani ya Lisaa Moja Tu na kila kitu kukamilika

Kwa sasa Kijana Wenu nimepona kabisa ugonjwa wa moyo uliokuwa unanisumbua kwa kipindi cha miaka yote na Jana jioni nimeruhusiwa kuendelea na mapumziko nyumbani na baada Ya Wiki 1 niweze kuendelea na majukumu yangu ya kila siku ..

Shukrani zangu nyingi za dhati zikufikie Popote Ulipo Mheshimiwa Rais wetu Tanzania Mama Yangu @samia_suluhu_hassan Asante sana Mama chini ya Utawala wako yanawezekana ambayo niliaminishwa hayatawezekana hadi niende India.. Asante Sana Mama Kijana wako Sasa ni Mwenye Afya iliyo ngangari na nakuahidi nitashikamana na wewe Mkoa kwa Wilaya , Vijiji kwa vitongoji kuhakikisha natangaza sifa za utendaji wako wa Kazi

Asante sana katibu mtendaji wa Basata @kmapana kwa mchango wako mkubwa kwenye kufanikisha hili

Shukrani zangu zikufikie Mkurugenzi Mkuu JKCI Dokta . PETER KISENGE kwakuwa na mimi Bega kwa Bega kuhakikisha natibiwa vizuri na napona Kabisa wewe sambamba na Madaktari na Wauguzi wote wa JKCI Muhimbili mlifanya hospital nipaone tu kama nipo nyumbani

Asante Sana Mashabiki Zangu Wote Kwa Dua Zenu 🤲🏽

"Sasa nimepona na kazi inendelee"💪🏾 ameandika msanii huyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet