Mbosso na Yammy kama Sharuk Khan na Kajol
Sisti Herman
June 13, 2024
Share :
Wanamuziki wa Bongo Fleva nchini Mbosso na Yammi wamejifananisha kama waigizaji kutoka nchini India Shah Rukh Khan na Kajol, hii ni baada ya kuachia video wakiwa chooni.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Mbosso ame-share video akiwa na Yammi ikiambatana na ujumbe usemao ‘Sharukhan & Kajol’ huku ikisikika sauti ya Mbosso katika wimbo wa ‘Ni Busu’ wa Barnaba aliyomshirikisha Yammi.
Imeelezwa kuwa Yammi, Mbosso na Barnaba tayari wameshafanya 'remix' ya ngoma hiyo iliyotoka mwezi mmoja uliyopita huku video yake ikiwa na zaidi ya watazamaji Elfu Sabini.