pmbet

Mbowe, Lissu kwenye 'Operation GF' ya siku 21 wakitumia 'Chopa'

Eric Buyanza

June 21, 2024
Share :

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Makamu wake, Tundu Lissu, kuanzia Juni 22, 2024 (kesho ) wanaanza opresheni ya mikutano ya kukijenga chama itakayofanyika kwa wiki tatu (siku 21) mfululizo katika mikoa ya Kaskazini wakitumia Helikopta 'Chopa' . 

Ziara hiyo iliyobatizwa jina 'Grassroot Fortification (GF)' inatarajiwa kugusa majimbo 35 na itaongozwa na mwenyeji wao, Godblesas Lema.

Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, alisema katika majimbo ya Ngorongoro na Karatu kutafanyika mikutano mitano kila jimbo na viongozi wote wakuu, Mbowe na Lissu watanguruma jukwaa moja.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet