Mbunge agoma kutaja bei ya saa yake, akiogopa kufukuzwa kazi
Eric Buyanza
July 24, 2024
Share :
Wakenya wengi wamekuwa na hasira kutokana na maisha ya juu ambayo viongozi wa umma wamekuwa wakiringishia kwenye mitandao ya kijamii.
Hali hiyo imezua mzozo baina ya wananchi hao wanaoishi maisha duni na viongozi wanaoonyesha mitandaoni mitindo mbalimbali ya mavazi na magari ya kifahari.
Hilo limesababisha baadhi ya viongozi kuishi kwa tahadhari kubwa, kwa mfano aliyekuwa mtangazaji maaarufu na Mbunge wa Lang’ata nchini Kenya, Phelix Odiwuor almaarufu kwa jina la 'Jalang’o' hivi majuzi amekwepa kujibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari aliyetaka kujua thamani au bei halisi ya saa yake ya mkononi.
Mbunge huyo aligoma kutoa jibu huku akimuuliza mwandishi, Unataka nifukuzwe kazi?
“Unataka nifukuzwe kazi? Hii saa, si ya bei kubwa sana ni kiasi tu,” alisema Jalang’o.
Mbunge huyo anafahamika kwa kuvaa saa za bei mbaya.
TAIFALEO