Mbunge aliyevua nguo Bungeni ili kutetea wanyonge
Eric Buyanza
June 4, 2024
Share :
December 11 mwaka 2013 huko nchini Mexico, Mbunge wa Chama cha PRD (Party of the Democratic Revolution) aitwae Antonio Garcia Conejo, alitoa kali ya mwaka wakati wa majibizano Bungeni baada ya kuamua kuvua nguo kama ishara ya kupinga muswada uliopitishwa ambao ulikuwa ukiruhusu makampuni ya kigeni kuwekeza katika sekta ya mafuta baada ya miaka 75 ya udhibiti wa serikali.
"Mnaona aibu kuniona nikiwa uchi lakini hamuoni aibu kuona watu wa mtaani wakiwa uchi, wamekata tamaa, hawana kazi na wana njaa baada ya kuwaibia fedha na mali zao”