pmbet

Mbunge ashambuliwa kwa kujisifu kwa ujenzi wa daraja hili

Eric Buyanza

May 7, 2024
Share :

Huko nchini Uganda Mbunge wa Ndorwa Mashariki, Mhe. Protazio Begumisa kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) ametupia picha ya daraja alilotengeneza kwa ajili ya wapiga kura wake.

Picha hiyo inamuonesha Mheshimiwa akiwa amepiga picha kwa majivuno kabisa akiwa juu ya daraja hilo la miti.

Kupitia huo aliandika;

"Watu wa Ndorwa Mashariki sasa wanaweza kutumia daraja la Rubira ambalo nimelitengeneza hivi karibuni," 

Hata hivyo tofauti na mategemeo yake, wengi waliibuka na kumshambulia kwa maneno makali wakimwambia anapaswa kujisikia aibu kwa hicho anachojisifia nacho.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet