pmbet

Mbunge ataka tozo ya sh 2,000 kwenye mitandao ya simu ili kuinusuru NHIF

Eric Buyanza

April 6, 2024
Share :

Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby, ameiomba serikali kuweka tozo ya Shilingi 2, 000 kwa mwezi katika mitandao ya simu pamoja na mazao ili kuusaidia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuendelea kujiendesha na kuwahudumia wananchi ipasavyo. 

Akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2024/25, Shabiby alisema hatua hiyo itakuwa mkombozi kwa mfuko huo ili kuondoa malalamiko ya mara kwa mara. 

“Kwa hili wanaweza kulikubali au wasilikubali wengine watatukana kwenye mitandao, lakini acha watukane maana kuna watu hawapo duniani na hata mbinguni hawako. 

Wako  katikati wanaelea, lakini siwezi kuogopa kwa sababu mtu atatukana. Alitaja njia za kupata chanzo hicho cha uhakika kuwa ni pamoja na kuweka tozo katika mitandao ya simu ambayo inatumiwa sana nchini, zikiwapo zaidi ya laini milioni 72. 

Alisema ikiwekwa tozo ya Sh. 2,000 kwa mwezi kwa mwaka itakuwa Sh. 24,000 sawa na Sh. trilioni 1.728 kwa idadi ya laini hizo. Mbunge huyo alishauri pia watumiaji wa mitandao hiyo wenye hadhi kama vile wabunge, wafanyabiashara, wafanyakazi kiwango kiongezwe hadi Sh.10,000 au 15,000 na kuunganishwa na kupatikana zaidi ya Sh.trilioni mbili. NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet