Mbwa ana uwezo wa kugundua magonjwa kwa wanadamu
Eric Buyanza
April 25, 2026
Share :

Huenda ukawa hujawahi kusikia hili lakini taarifa ikufikie kuwa mbwa maalum aliyefunzwa ana uwezo mkubwa wa kutambua magonjwa mbalimbali yanayomsumbua binadamu kwa kunusa tu.
Baadhi ya magonjwa hayo ni saratani ya kibofu cha mkojo, malaria, kifafa, kisukari na hata saratani.
Inaaminika uwezo wa mbwa wa kunusa harufu, ni mara 10,000 zaidi ya uwezo wa binadamu, hivyo wana uwezo wa kugundua mabadiliko madogo katika mfumo wa harufu kupitia kemikali za mtu. Wanaweza kutambua mabadiliko madogo katika kemikali ambayo mwili hutoa kwa viwango vya chini sana, hata wakati mtu akiwa na afya.
Pumzi ya mwanadamu inatoka takribani kemikali za gesi 3,500. Muundo na mkusanyiko wa kemikali ambazo mwili hutoa hubadilika kulingana na afya ya mtu na kemikali hizo hubadilika ikiwa mwili unapigana na maambukizi au kukabiliana na tatizo la kiafya.
Mfano, mbwa wa kugundua uviko 19, walikuwa wepesi na bei nafuu kuliko vipimo vya kawaida vya PCR. Kwa kuelewa uwezo wa wanyama, tunaweza kuboresha uchunguzi wa maabara.
Ingawa kutumia ujuzi wa kunusa wa wanyama kunaweza kuwa na manufaa kwetu, ni muhimu kukumbuka kwamba afya na ustawi wa viumbe hawa lazima pia vipewe kipaumbele.





