Mbwa wa Joe Biden atafuna walinzi wa Ikulu
Eric Buyanza
February 22, 2024
Share :
Mbwa wa Rais Joe Biden wa Marekani, ameshawauma au kujeruhi walinzi wa Rais huyo zaidi ya mara 24 kabla ya kuondolewa kwenye makazi hayo ya Ikulu ya White House.
Nyaraka mpya zilizotoka kwa umma hivi karibuni zilionyesha kuwa Mbwa huyo aina ya German Shepherd aliyepewa jina la (Kamanda) alisababisha baadhi ya walinzi hao kujeruhiwa maeneo mengi ya mwili ikiwemo mapajani, mkononi kwenye mabega na hata kifuani.
Mlinzi mkuu ambaye hakutajwa jina katika barua pepe moja alishauri kwamba walinzi wanaomlinda Bw Biden na familia yake lazima wawe wabunifu ili kuhakikisha usalama wao binafsi.
"Kung'atwa na mbwa kumetupa changamoto ya kurekebisha mbinu zetu za kufanya kazi wakati Kamanda yupo" ilisomeka barua pepe moja iliyovuja iliyoandikwa na mkuu huyo wa ulinzi.