pmbet

Mbwa wa polisi aingia chekechea, yaliyomkuta hatasahau

Eric Buyanza

July 3, 2026
Share :

Picha na video za mbwa wa polisi anayeitwa K-9 Rex zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii na kugusa mioyo ya watu wengi duniani baada ya mbwa huyo kupambwa kwa stika na watoto wa shule ya chekechea.

 

Tukio hili lilitokea wakati wa ziara ya kijamii ya jeshi la polisi kwenye shule hiyo.
 

Inaelezwa kuwa wakati askari aliyekuwa akimwongoza Rex akiongea na walimu, kundi la watoto liliamua kumfanyia Rex "urembo" wa siri.

 

Watoto hao walimbandika stika nyingi za nyota, moyo, na alama za kutabasamu.

 

Licha ya kwamba tunafahamu mbwa wa polisi hufundishwa kazi ngumu za kiusaama na huwa ni mkali sana, lakini Rex alikaa chini kwa utulivu mkubwa na kuacha watoto wacheze naye bila kuleta madhara yoyote.

 

Ripoti zinasema kuwa hata baada ya askari kujaribu kumwondolea stika hizo, Rex alionyesha kuzifurahia na hakutaka ziondolewe, jambo lililowachekesha wengi mitandaoni.

 

Tukio hili limepongezwa sana kama mfano mzuri wa jinsi mbwa wa polisi walivyofundishwa vizuri kuwa wapole na salama wanapokuwa karibu na watoto wadogo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet