pmbet

Mchazaji wa R.Betis amwaga machozi kisa kukatwa jina dakika za jioni.

Joyce Shedrack

September 2, 2026
Share :

Mchezaji Pablo Garcia mwenye umri wa miaka 20 aliyekulia katika akademi ya Real Betis, amezua gumzo baada ya kondoka katika klabu hiyo kwa huzuni kubwa baada ya kuuzwa siku ya mwisho ya usajili.

Real Betis wants to increase Pablo García's release clause | Fichajes.net

García alijiunga na Betis akiwa na umri wa miaka sita na ameitumikia takribani miaka 15 ikiwa ni klabu yake ya utotoni lakini cha kushangaza zaidi, alikuwa ameanza msimu huu vizuri, akicheza katika mechi zote tatu za Real Betis za LaLiga.

 

Wiki iliyopita, García alifunga bao la ushindi dakika za mwisho dhidi ya Valencia, lakini siku chache baadaye akaambiwa kuwa atalazimika kuondoka.

 

Kutokana na sheria kali za kifedha za LaLiga, Real Betis iliamua kumuuza García kwenda Racing Santander ili kupata nafasi ya kumsajili tena Dani Ceballos, ambaye alirejea klabuni hapo baada ya miaka tisa akiwa Real Madrid.

 

Uamuzi huo umeibua hasira na masikitiko makubwa kutoka kwa mashabiki wa Betis, ambao wamehoji namna klabu ilivyoshughulikia suala hilo.

 

García ameondoka Betis akiwa analia yeye pamoja na mama yake mzazi baada ya kucheza jumla ya mechi 33 za kikosi cha kwanza, akifunga mabao matatu.

 

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania chini ya miaka 21 sasa anatarajiwa kuanza ukurasa mpya akiwa Racing Santander, huku akitarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Rayo Vallecano.

 

Miaka 15 ya kuilinda jezi ya Betis, lakini mwisho wake ukawa ni machozi na kuondoka wakati ambao bado alikuwa anahitaji kuendelea kuitetea jezi ya timu iliyomtambilisha kwenye soka la kulipwa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet