Mchengerwa amtumbua Kaimu Mganga mkuu Kagera
Sisti Herman
December 17, 2023
Share :
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa ameagiza Utenguzi wa uteuzi wa Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Dkt. Issesanda Kaniki baada ya kupokea malalamiko kuhusu ukosefu wa huduma bora za Afya kwenye baadhi ya Vituo vya kutolea huduma na kauli zisizoridhisha kutoka kwa baadhi ya watoa Huduma za Afya.
Mnamo Novemba 27, 2023 mdau wa afya kupitia mitandao ya kijamii alilalamikia Kituo cha Afya cha Zamzam katika Manispaa ya Bukoba akidai hakina huduma nzuri kwa Wajawazito, Wahudumu kutojali wenye uhitaji, kuwapuuzia na kuwajibu vibaya na baadhi ya Watumishi kutengeneza mazingira ya Rushwa ili kutoa huduma ya haraka kwa Wanufaika wa Bima ya NHIF.