Mchezaji afungiwa kisa kukataa kusapoti mapenzi ya jinsia moja
Sisti Herman
May 31, 2024
Share :
Mchezaji wa Monaco Mohamed Camara raia wa Mali amefungiwa mechi nne za Ligi Kuu Ufaransa (LFP) baada ya kuziba nembo ya kusapoti ‘Mapenzi ya Jinsi Moja’ (LGBTQ+) kwenye Jezi yake kwenye mechi ya Ligue 1.
Mapema wiki iliyopita, Waziri michezo Amelie Oudea-Castera alisisitiza mchezaji huyo kupewa adhabu nzito kutokana na kukiuka maagizo hayo kwa kuziba nembo inayohamasisha mambo hayo kwenye mchezo dhidi ya Nantes ambapo walishinda 4-0 huku yeye akitupia goli moja kwa mkwaju wa penalti.