Mchezaji akataa kuliwakilisha Taifa lake kwenye Kombe la Dunia 2026.
Joyce Shedrack
May 25, 2026
Share :
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Haiti na klabu ya RC Lens ya Ufaransa Odsonne Édouard amezua gumzo baada ya kukataa nafasi ya kuiwakilisha Nchi yake kwenye mashindano ya Kombe la Dunia 2026.

Edouard mwenye umri wa miaka 28 ambaye amefunga 12 ktika michezo 29 ya ligi kuu ya Ufaransa amekataa kujiunga na kikosi cha Kombe la Dunia kilichoitwa na Shirikisho la Nchi yake baada ya Haiti kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974 huku akiweka wazi ni kwa sababu hakuwa sehemu ya kikosi kilichoisaidia Nchi yake kufuzu michuano hiyo
“Nisingejihisi kuwa nina haki ya kucheza Kombe la Dunia kwa sababu kulikuwa na wachezaji waliopigania kufuzu, na mimi sikuwa tayari kuja dakika za mwisho kunufaika na juhudi zao.”
“Kwa kifupi, kama nitacheza, basi ni lazima nistahili.”Amesema mshambuliaji huyo.





