Mchezaji apigwa na radi uwanjani
Sisti Herman
February 13, 2024
Share :
Katika tukio la kushangaza na la kusikitisha lilitokea wakati wa mechi ya mpira wa miguu kati ya 2 FLO FC Bandung na FBI Subang za nchini Indonesia iliyochezwa Jumapili, Feb 11, mchezaji alipigwa na radi na kuanguka.
Katika video ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii, mwanasoka anaonekana akitembea uwanjani, akisubiri mpira umfikie, ghafla radi ikampiga na mchezaji huyo kuanguka uwanjani na kuleta mshutuko kwa watu wengi uwanjani hapo.
Kulingana na ripoti ya vyombo vya habari nchini humo, mchezaji huyo alipelekwa hospitalini mara moja lakini hakunusurika kwani alishafariki.