pmbet

Mchezaji asimamishwa Uturuki kisa kuwataja mateka wa Israel

Sisti Herman

January 15, 2024
Share :

Mchezaji wa Soka ambaye ni Raia wa Israel Sagiv Jehezkel anayeichezea Club ya Antalyaspor ya Nchini Uturuki, amesimamishwa na Club hiyo baada ya kushangilia goli alilofunga dakika ya 68 kwenye mechi dhidi ya Club ya Trabzonspor kwa kuonesha upendo wake kwa Waisrael na Watu wengine wanaoshikiliwa mateka na Hamas kwa siku 100 sasa ambapo ameli-dedicate goli hilo kwao.

Baada ya kufunga goli hilo Sagiv aliisogelea camera na kuonesha bendeji yake ikiwa imeandikwa ‘siku 100 . October 7’ akiashiria kuwa Mateka hao wanafikisha siku 100 sasa tangu wawe chini ya Hamas walipotekwa kwenye shambulio la October 07,2023 na kama ishara ya kutaka waachiwe.

Saa moja baada ya mchezo huo, Club hiyo ilitoa tangazo kwenye ukurasa wake wa X (zamani Twittter) ikiaema imemsimamisha Mchezaji huyo mpaka itakapotoa taarifa nyingine, hiyo ni baada ya Waturuki wengi kuonesha kukerwa na kitendo hicho “Club haiwezi kuruhusu vitendo ambavyo vinakwenda kinyume na maslahi ya Taifa letu”

Baadaye Club hiyo ikatoa pia taarifa kutoka kwa Rais wa Club Sinan Boztepe ambaye amelaani kitendo hicho na akisema hawezi kukubali kufanyika kwa vitendo kama hivyo akiwa Rais wa Club.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet