Mchezaji atembezewa bakora na shabiki baada ya timu kufungwa
Eric Buyanza
April 16, 2024
Share :
Shirikisho la Soka la Saudi Arabia limesema litakagua upya kanuni za maadili za mashabiki baada ya shabiki mmoja nchini humo kumtandika bakora mchezaji Abderrazak Hamdallah wa Al-Ittihad.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa mchezo baada ya Al-Ittihad kufungwa na Al-Hilal katika michuano ya Saudi Super Cup mjini Abu Dhabi.
Katika taarifa yake Shirikisho la Soka la Saudi Arabia lilisema limeshtushwa sana na tukio hilo la aibu.
"Kandanda nchini Saudi Arabia ni mchezo wa familia na, tunashukuru, machafuko ya mashabiki ni nadra sana," ilisema taarifa hiyo......"Vitendo vya shabiki huyu vinaenda kinyume na yote ambayo soka la Saudia linawakilisha na tunalaani vikali tukio hilo......"Kutakuwa na ukaguzi wa kina wa maadili ya mashabiki......ukaguzi huo utahakikisha sheria na kanuni zilizoboreshwa zinawekwa ili kutoa adhabu kwa haraka ili kuzuia kurudiwa kwa matukio kama haya." ilimazia taarifa hiyo.