pmbet

Mchezaji Lucas Trejo ampoteza mke na watoto kwenye tetemeko.

Joyce Shedrack

June 29, 2026
Share :

Mchezaji wa soka raia wa Argentina anayekipiga katika timu ya daraja la pili nchini Venezuela amepoteza mke wake na watoto wake wawili kufuatia matetemeko ya ardhi ya wiki iliyopita, ambayo yalikuwa yenye nguvu zaidi kuikumba Venezuela katika kipindi cha zaidi ya karne moja.

Soccer Star's Wife and 2 Kids Found Dead After 72-Hour Search

Lucas Trejo, ambaye anachezea klabu ya Sport Marítimo La Guaira, alitumia sehemu kubwa ya siku tatu zilizopita akichimba kwenye vifusi na kutafuta dalili zozote za mke wake, Yanina, pamoja na watoto wao Aarón na Ainhoa.

 

Trejo mwenye umri wa miaka 38 alikuwa katika kambi ya mazoezi ya timu yake mjini Caracas wakati matetemeko hayo mawili yalipotokea, baada ya janga hilo alikimbilia nyumbani kwake huko La Guaira, umbali wa takriban kilomita 29 kaskazini mwa mji mkuu ili kuitafuta familia yake na kukuta jengo la nyumba yake limeanguka lote.

 

"Alichokikuta kilikuwa ni tukio la kutisha sana,"Hakukuta chochote kabisa kilichokuwa kimebaki cha jengo lenyewe. Tumaini letu lilikuwa kwamba hawakuwa ndani wakati jengo hilo lilipoanguka."Amesema kaka yake Trejo.

 

Zaidi ya watu 1,400 walifariki dunia, huku maelfu wengine wakiripotiwa kutoweka nchini Venezuela, mamlaka zilisema Jumapili.

 

 

 

 

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet