Mchezaji wa Nigeria akwama nchini Qatar kufuatia anga kufungwa
Eric Buyanza
March 2, 2026
Share :

Nahodha wa zamani wa Super Eagles William Troost Ekong ni mmoja wa nyota kadhaa wa kimataifa ambao wamekwama nchini Qatar wakati huu ambapo kuna mgogoro wa kivita Mashariki ya Kati.
Ekong amekwama kufuatia mvutano na mashambulizi ya kijeshi kati ya Iran na Israeli na mshirika wake Marekani, mvutano ambao umelazimisha mamlaka kufunga anga la nchi hiyo.
Beki huyo wa Nigeria, ambaye hivi karibuni alijiunga na timu ya Ahli SC ya Ligi ya Qatar, hawezi kuondoka nchini humo baada ya wasiwasi wa usalama kusababisha kusimamishwa kwa safari za ndege na shughuli za mpira wa miguu.





