Mchezaji wa Senegal Afariki akiwa uwanjani.
Joyce Shedrack
February 23, 2026
Share :
Soka la Senegal ipo katika maombolezo kufuatia kifo cha ghafla cha mshambuliaji wa AS Saloum, El Hadji Youssou Diouf aliyefariki baada ya kupata dharura ya kiafyya akiwa uwanjani.

Mshambuliaji huyo alifariki dunia Jumapili, Februari 22, mjini Thiès baada ya kushiriki katika mechi ya raundi ya 16 kati ya Saloum na Amitié FC.
“Mchezaji huyo alishiriki katika mechi kati ya Amitié FC na AS Saloum na alicheza takribani dakika ishirini wakati wa raundi ya 16 ya michuano. Alitolewa uwanjani katika dakika ya 72, na baada ya filimbi ya mwisho huku akiwa amekaa kwenye benchi la wachezaji wa akiba, alipata dharura ya kiafya. Hakuwa anafunga wakati tukio hilo lilipotokea.”Imesema taarifa ya hiyo.





