Mchungaji aliyemwita Rais 'Pepo' aachiwa huru
Eric Buyanza
July 9, 2024
Share :
Mchungaji na Waziri wa zamani wa sheria wa Equatorial Guinea, ambaye aliwekwa kizuizini miaka miwili iliyopita kwa kumwita Rais "pepo", ameachiwa huru.
Rubén Maye Nsue Mangue aliachiwa huru baada ya kusamehewa na Rais Teodoro Obiang Nguema.
Bw Mangue alikamatwa kwa kumkosoa Rais Teodoro kupitia sauti iliyosambaa sana kwenye mitandao ya kijamii mwaka 2022, akimuita "pepo... kwa kuwashikilia watu wake kama wafungwa".
Alikataa kuomba msamaha kwa mkuu wa nchi, hatua ambayo ilimfanya kufunguliwa mashtaka kwa kuchochea ghasia.
Bwana Mangue alikuwa Waziri wa sheria kuanzia 1998 hadi 2004 alipofutwa kazi kufuatia tofauti kati yake na rais.
Rais Teodoro Obiang mwenye umri wa miaka 82, ndiye mtawala aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika, baada ya kuchukua madaraka mwaka 1979.
BBC