pmbet

Mchungaji maarufu anusurika jaribio la mauaji

Eric Buyanza

January 3, 2024
Share :

Mchungaji wa kanisa la House of Prayer Ministries International na mfanyabiashara maarufu nchini Uganda, Aloysius Bugingo amenusurika kifo wakati wa shambulio la watu wasiojulikana na kupelekea kuuwawa kwa mlinzi wake katika mji mkuu wa Kampala.

Watu hao wenye silaha walilifyatulia risasi gari la Mchungaji Bugingo alipokuwa akienda nyumbani kwake Jumanne usiku katika eneo la Namungoona.

Washambuliaji hao baadaye walitoroka eneo la tukio kwa pikipiki.

Licha ya kupata majeraha wakati wa shambulio, Bugingo alifanikiwa kuliendesha gari hilo hadi hospitali iliyo karibu, polisi walisema.

Mlinzi wa mchungaji huyo, Richard Muhumuza, alifariki dunia kutokana na majeraha ya risasi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet