Mdukuzi asimulia alivyodukua mifumo ya Man City na kupata taarifa zao za siri
Sisti Herman
October 5, 2026
Share :

Mdukuzi wa mitandao Rui Pinto raia wa Ureno amesimulia namna alivyoweza kudukua na kupata taarifa za siri za klabu ya Manchester City zilizopelekea kukutwa na hatia ya mashtaka 115 ya matumizi mabaya ya fedha.
"Ilikuwa ni barua pepe iliyoonekana haina madhara yoyote, iliyotumwa asubuhi ya Jumatano mwezi Januari 2017, ndiyo iliyoanzisha kila kitu"
"Ilipowasili kwenye kikasha cha barua pepe cha afisa mwandamizi wa Manchester City, ilionekana kama imetumwa na mfanyakazi wa shirikisho linalosimamia soka barani Ulaya (UEFA), na ilikuwa na kiungo cha ripoti ya utiifu wa kanuni za kifedha".
"Afisa huyo wa City alibofya kitufe cha kupakua. Hicho ndicho kilichohitajika tu".
Haikuwa barua pepe halisi kutoka UEFA, bali jaribio lililofanikiwa la wizi wa taarifa nyeti (phishing) lililofanywa na mdukuzi na mwanaharakati kutoka Ureno, Rui Pinto.
Mifumo ya kompyuta ya City ilivamiwa, jambo lililomwezesha Pinto kupata maelfu ya barua pepe na nyaraka kutoka kwenye mifumo ya klabu hiyo.
Wiki hii, takriban miaka 10 tangu kutumwa kwa barua pepe hiyo ya awali ya Pinto, Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League) ilitangaza kuwa jopo huru limewakuta City na hatia katika mashtaka yote dhidi yao isipokuwa moja, kama ilivyoripotiwa na The Athletic





