pmbet

Mechi 3, alama 3...! Yanga yarejea kinyonge jiji la Masimango

Sisti Herman

March 22, 2026
Share :

 

Baada ya kuvuna alama 3 kwenye mechi 3 za ugenini, sawa kikosi cha Wananchi Yanga kimerejea nyumbani jijini Dar es salaam kikotokea jijini Dodoma.

Yanga imeangusha alama 6 kwenye mechi hizo 3 walizokuwa na malengo ya kuvuna alama 9 baada ya 'kushona' sare 3 mfululizo dhidi Azam FC, TRA United na jana Mtibwa Sugar.

Yanga kupitia msemaji wao @alikamwe wamedokeza kuwa wanachukua mapumziko ya mechi za kimataifa za FIFA kama sehemu ya kufanya tathmini ya kina kujua 'wapi panavuja' ili wapafanyie mabaoresho.

Je unadhani wapi panavuja pale kwa wananchi?

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet