Mechi ya 1 dakika 30 bila kugusa mpira mechi ya 2 dakika 24 chuma 2 na Assist 1.
Joyce Shedrack
June 22, 2026
Share :
Mshambuliaji wa Hispania Mikel Oyarzabal amekuwa na mchezo wa kihistoria wa kurejea kwa nguvu baada ya kipindi kigumu usiku wa jana Baada ya kuweka rekodi ambayo asingependa kuikumbuka katika mechi ya kwanza ya Hispania dhidi ya Cape Verde alipokuwa mchezaji wa kwanza tangu mwaka 1966 kucheza dakika 30 za mwanzo bila kugusa mpira hata mara moja.
Kwenye mchezo wa pili wa Kombe la Dunia siku ya jana ameweka historia nyingine kwa kufanya comeback ya kipekee kutokana na kiwango kikubwa alichokionesha dhidi ya Saudi Arabia kwa kufunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao ndani ya dakika 24 pekee.
Maana halisi ya nyakati ngumu hazidumu milele jana Oyarzabal amelisaidia Taifa lake kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 na kuvuna alama 3 za kwanza katika michuano hiyo.





