Mechi ya TRA dhidi ya Simba kupigwa Arusha
Sisti Herman
March 12, 2026
Share :

Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya TRA United na Simba SC utapigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha
Hayo yamebainishwa na Ofisa habari TRA United, Christina Mwagala akitoa taarifa kwa vyombo vya habari.
TRA iliuchagua uwanja wa Black Rhino, Karatu kama uwanja wao wa nyumbani na jana ilicheza dhidi ya Namungo na kupata ushindi wa mabao 2-0.
Kutokana na ukubwa wa mchezo huo klabu imetangaza kutumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid badala ya Black Rhino.
Aidha, Christina ameongeza kuwa jana baada ya timu hiyo kupata ushindi, mara moja ilianza maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba wakihitaji kupata ushindi kwenye mchezo huo.
TRA United v Simba utapigwa saa 10:00 Jioni, Machi 14, 2026.





