pmbet

Meek Mill achoshwa na maisha ya Marekani, afikiria kuhamia Ghana

Eric Buyanza

March 9, 2024
Share :

Rapa wa Marekani, Meek Mill, amekuwa gumzo kwenye vyombo mbalimbali vya habari duniani, safari hii kwa kutangaza nia yake ya kuutaka uraia wa Ghana.

Katika tweet aliyoichapisha kwenye ukurasa wake Machi 4, 2024, Meek Mill alitaja unyanyasaji wa watu Weusi huko Marekani kama sababu kuu nyuma ya uamuzi wake.

Tamko hili linakuja baada ya ziara ya kwanza kabisa ya Meek Mill nchini Ghana mwaka 2022, alipotumbuiza katika tamasha la 'Afro-Nation' na kuelezea jinsi anavyoipenda nchi hiyo.
 

Wakati wa ziara yake, alipata fursa ya kutembelea Ikulu ya nchi hiyo (Jubilee House) na kufanya mazungumzo na Rais Akufo-Addo.

Tangu wakati huo mapenzi yake kwa Ghana yamekuwa yakiongezeka ambapo mapema mwaka huu alionyesha nia ya kushirikiana na wasanii wa nchi hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet