Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge afariki Dunia.
Joyce Shedrack
October 12, 2024
Share :
Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge amefariki dunia leo October 12,2024 alfajiri akiwa Nchi India alipokuwa akipatiwa matibabu, kifo cha Mbuge kimethibitishwa na Mtoto wake.
August 02, 2024 Mbuge aliagwa rasmi Jeshini baada ya kulitumikia Jeshi kwa zaidi ya miaka 38 na aliagwa kwa kukagua gwaride rasmi la kijeshi katika Viwanja vya Mgulani (Twalipo Admistration Unit-TAU) Jijini Dar es salaam.
Mbuge amepitia katika nafasi mbalimbali za Uongozi ikiwemo kuwa Mkuu wa JKT, Mkuu wa Mkoa Kagera na Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu.