Meli yenye watalii 2200 yatia nanga bandari ya DSM
Sisti Herman
January 16, 2024
Share :
Meli yenye urefu wa mita 294 kutoka kampuni ya Norwegian Dawn nchini Norway imetia Nanga katika Bandari ya Dar es salaam ikiwa imebeba watalii 2200 kutoka Ulaya. Meli hiyo imetia nanga katika bandari hiyo ikiwa ni matokeo ya mradi wa kuongeza kina cha maji na ujenzi wa gati.