pmbet

Messi afukuzia rekodi ya Ronaldo afikisha magoli 840.

Joyce Shedrack

September 16, 2024
Share :

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Argentina na klabu ya Inter Miami ya Marekani  mwenye umri wa miaka 37 Lionel Messi amefikisha mabao 840  katika maisha yake ya soka siku ya jana baada ya kufunga mabao mawili na kupika moja timu yake ya Inter Miami ikishinda 3-1 dhidi ya Philadelphia kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka ya Marekani.

Katika maisha yake ya soka Messi amecheza mechi 1070 akifunga mabao 840 na kutengeza mengine akitoa pasi za mwisho (asissts) 375 na kumfanya kuhusika kwenye jumla ya magoli 1215.

 

Mwaka 2011 na 2012 ilikuwa miaka bora sana kwa mchezaji huyo kwani alifanikiwa kuingia kambani mara nyingi zaidi kwa kufunga mabao 60 mwaka 2011 na 2012 kufikisha mabao 91.

Kwa mwaka huu mpaka sasa Messi ana mabao 19 aliyoyafunga kwenye Timu ya Taifa pamoja na kwenye klabu yake huku mwaka uliopita akishindwa kufikisha mabao 30 baada ya kufunga mabao 28 pekee.

 

Ikumbukwe kuwa siku chache zilizopita,Cristiano Ronaldo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa kiume katika historia kufunga magoli 900 kwenye mechi rasmi baada ya kufunga goli katika mechi ya UEFA Nations League kati ya Ureno na Croatia iliyochezwa Lisbon wiki moja iliyopita

 

Je unadhani Messi atastaafu soka akiwa na magoli mangapi ?.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet