pmbet

Messi alambwa faini kwa kumpiga Sullivan kibao cha kisogo

Eric Buyanza

August 22, 2026
Share :

Kamati ya Nidhamu ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS) imemtoza faini nahodha wa Inter Miami, Lionel Messi, kwa kosa la kumpiga kibao cha kisogoni mchezaji wa Philadelphia Union, Quinn Sullivan.

 

Mchezo huo uliochezwa Jumatano, Agosti 19, 2026, uliisha kwa sare ya 2-2. Tukio hilo lilitokea katika dakika ya 101 ya mchezo (muda wa nyongeza).

 

Messi alikasirishwa na Sullivan baada ya kuhisi kuwa mchezaji huyo alimpiga kiwiko kufuatia pasi aliyopiga, jambo lililomfanya Messi kumsukuma Sullivan na kumpiga kibao cha kisogo wakati wakizozana kwa maneno.

 

Kitendo hicho kimevunja sheria ya MLS inayokataza wachezaji kuwashika wapinzani wao sehemu za uso, kichwa, au shingo.

Hata hivyo kamati hiyo ya nidhamu haikuweka wazi kiasi kamili cha fedha ambacho Messi ametozwa kama faini.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet