Messi amekuwa mwanasoka wa kwanza kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA kwa mara ya tatu
Eric Buyanza
January 16, 2024
Share :
Lionel Messi amekuwa mwanasoka wa kwanza kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA kwa Wanaume kwa mara ya tatu.
Messi mwenye miaka 36, alithibitishwa kuwa mshindi wa tuzo hizo za mwaka huu 2023 katika hafla zilizofanyika London Uingereza usiku wa kuamkia leo.
Hata hivyo, Messi hakuwepo kwenye tafrija hiyo kwani alikuwa na wachezaji wenzake wa Inter Miami wakijiandaa na mechi ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya dhidi ya El Salvador siku ya Ijumaa.
Messi ameshinda tuzo hiyo baada ya kuongoza kwenye kura zilizopigwa akiwashinda Erling Haaland pamoja na Kylian Mbappe.
Nahodha huyo wa Argentina amewahi kushinda tuzo hiyo mwaka 2019 na 2022.
Tuzo Bora la FIFA humtambua mchezaji bora zaidi katika mchezo wa wanaume kila mwaka.
Angalizo: Picha iliyotumika hapo ni ya tuzo za 2022.