Messi amkumbuka Maradona baada ya ushindi wa Argentina
Eric Buyanza
July 16, 2026
Share :

Nahodha wa Argentina, Lionel Messi, amemuenzi gwiji wa soka wa nchi hiyo, Diego Maradona, akisema anaamini kuwa anasherehekea ushindi wa Argentina akiwa mbinguni.
Messi amesema mafanikio hayo ni zawadi maalumu kwa Maradona na siku ambayo itaendelea kukumbukwa.
"Hakika Diego anafurahia ushindi huu akiwa juu mbinguni. Hii ni zawadi kwake pia, na ni siku ya kipekee sana," alisema Messi.
Akizungumzia ushindi wa Argentina wa mabao 2-1 dhidi ya England katika mchezo wa nusu fainali, Messi alisema kurejea kwa timu hiyo kulijengwa katika mtindo wao wa kawaida wa kucheza, uliotawaliwa na uvumilivu, utulivu na umiliki mzuri wa mpira.
Alieleza kuwa licha ya kuruhusu bao, wachezaji waliendelea kuwa watulivu, walitengeneza nafasi nyingi za kufunga na kuendelea kuamini mfumo wao wa mchezo ambao umewaletea mafanikio kwa miaka mingi.





