Messi amtaja kinda wa Arsenal, kwenye orodha ya mastaa wa baadaye
Eric Buyanza
October 12, 2026
Share :

Kalamu ya mshambuliaji nguli wa soka duniani, Lionel Messi, imemgusa kijana chipukizi wa Arsenal, Max Dowman (16), baada ya kumjumuisha katika orodha ya wachezaji 10 bora chipukizi duniani wa kuwaangalia kwa karibu.
Uteuzi huo umefanyika kupitia msimu wa tatu wa kampeni maarufu ya kibiashara ya "Messi +10" inayoratibiwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas, ambapo nahodha huyo wa Argentina alitakiwa kuchagua vijana wenye umri chini ya miaka 21 wanaotajwa kuwa na mustakabali wa kuwa mastaa wakubwa.
Dowman, ambavyo amekuwa akionyesha kiwango kikubwa katika akademi ya Arsenal na kupandishwa kikosi cha kwanza msimu huu, amepata sifa hiyo ya kipekee huku mtindo wake wa uchezaji ukifananishwa na Messi mwenyewe kutokana na uwezo wake wa kupenya ngome za walinzi kwa kasi na chenga.





