Messi anakuwa mchezaji mwenye mataji mengi zaidi katika historia ya soka
Eric Buyanza
July 15, 2024
Share :
Nahodha wa Argentina, Lionel Messi, ameingia kwenye rekodi ya kuwa mchezaji mwenye mataji mengi zaidi katika historia ya soka.
Messi alicheza kwa dakika 60 alfajiri ya leo wakati nchi yake ilipoilaza Colombia 1-0 katika fainali ya Copa America 2024.
Taji la leo linakuwa la 45 kwa mchezaji huyo kushinda katika maisha yake ya soka.
Messi mwenye umri wa miaka 37 anavunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona Dani Alves (44).