"Messi anastahili kushinda Ballon D'Or hilo halina mjadala"-De Paul.
Joyce Shedrack
September 19, 2026
Share :
Kiungo wa Argentina, Rodrigo De Paul, ametoa kauli ya wazi kuhusu mjadala wa Ballon d’Or, akisisitiza kuwa kwa mtazamo wake hakuna mjadala kuhusu Lionel Messi kuwa mshindi.

De Paul amesema kuwa katika mwaka ambao kuna Kombe la Dunia, hakuna mchezaji aliyewahi kufanya kile ambacho Messi alikifanya, licha ya kuwa na umri wa miaka 39.
“Kwangu mimi, hakuna mjadala kabisa. Katika mwaka ambao kuna Kombe la Dunia, hakuna mtu aliyewahi kufanya na hakuna atakayefanya kile ambacho Messi alifanya, akiwa na umri wa miaka 39.”
De Paul ameongeza kuwa Messi alivuka mipaka yote, akashindana dhidi ya wachezaji bora wa vizazi tofauti na kuonyesha kiwango cha kipekee kwenye Kombe la Dunia.
“Alivuka kila kikomo, akashindana dhidi ya wachezaji wa kipekee wenye umri tofauti, na alikuwa mchezaji bora kwenye Kombe la Dunia. Hakuna mjadala.”Amesema De Paul.





