pmbet

Messi anatoka sayari nyingine, alizaliwa ili kucheza soka - Okocha

Eric Buyanza

August 18, 2026
Share :

Aliyekuwa nahodha wa Super Eagles, Austin ‘Jay Jay’ Okocha, amemchagua nahodha wa Argentina, Lionel Messi, kuwa mchezaji bora wa muda wote akimuacha pembeni nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo.

 

Okocha alitoa kauli hiyo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha The Obi One Podcast kinachoendeshwa na John Obi Mikel.

"Kwangu mimi, ni Messi. Ronaldo ni wa kipekee, lakini yeye ni mfungaji wa mabao kama Haaland.

 

"Messi anatoka sayari nyingine. Alizaliwa ili kucheza soka. Nadhani Messi angeugua kama asingekuwa akicheza soka," alisema Okocha.

Messi na Ronaldo walitawala ulimwengu wa soka kwa zaidi ya muongo mmoja na kushinda jumla ya tuzo 13 za Ballon d’Or kati yao.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet